Uchaguzi 2020 Wafahamu watu 75 waliokuwa wabunge wa CCM walioliwa kichwa na kukosa uteuzi. Wamo Mwakyembe, Tizeba, Nkamia, Chenge, Adadi, Ngeleja, Masele nk

Habari haijaa uongo bali ina mapungufu machache sana kama hao wawili tu na kukosekana jina la Steven wasira mle
Steven Wasira hakuwa Mbunge wa Bunge linalomaliza muda wake
 
Halima bulembo niliona kama kashinda. Anyway kiutaniutani na miujiza Gwajima anachukua jimbo la kawe.

Kuna yule mtoto wa marehemu Kigoda . Omary kigoda alikuwa mbunge huko Handenj sijui kapita???
 
Hicho kitu ndiyo bado kinaniuma sana naomba maana ataanza kutusumbuwa sana na kutukomoa Tena maana Ile bichwa inapenda misifa sana,, Naomba Raisi ampotezee mazima🤔🤔🤔
Watanzania wanataka katiba mpya izuie wabunge wa kuteuliwa na Rais kuwa mawaziri kwani Rais hutumia vibaya vile viti 10 kuwateua washikaji zake kisha kuwazawadia uwaziri kienyeji sana
 
Pitia upya hii orodha, kuna Sixtus Mapunda, na Ngonyani walishinda kura za maoni lakini wamekatwa
 
M
Mwakyembe na Bashite Bora wasipewe kitu chochote kabisa wazinguwaji sana Hawa jamaa
Bashite anatafutiwa cheo kwa udi na uvumba hata mpambe wake Le mutuz katoa siri kuwa wanakesha makanisani na kwa waganga wa kienyeji masaa mengi ili Bashite apate cheo na wao wanufaike kupitia mgongo wake kama kawaida yao.
 

Sixtus Mapunda ( Mbinga Vijijini)
 
Hahahaha hahaaaa kelele zote za Juma Nkamia za kujipendekeza zimegonga mwàmba
 
Wengine hapo hawakutia nia.
 
Atateuliwa kuwa DAS
Mtukufu atawazawadia vyeo wale CCM wote walioongoza kura za maoni na wale wakiokuwa wa pili tatu nne, CCM ni ile ile mambo ni yaleyale
 
Pale kwa kumkata mpigania mambo Mkaa100 wamenifurahisa sana.
 
Hahahaha hahaaaa kelele zote za Juma Nkamia za kujipendekeza zimegonga mwàmba
Juma Nkamia CCM wenzake wamefurahia kupigwa chini kwani huwa wanamuona kama mbunge kihere here mjuaji mno mpaka kapitiliza, CCM nao hawawapendi washambenga mipasho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…