The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
Katika simulizi ya kusisimua ya mwisho wa maisha ya Yesu hapa duniani, tunawaona watu wawili wa kipekee: Yusufu wa Arimathaya na Nicodemus. Hawa si watu wa kawaida walikuwa watu wa heshima kubwa, wanachama wa baraza la Sanhedrin (baraza kuu la wayahudi), lakini pia walikuwa wanafunzi wa Yesu kwa siri kwa sababu ya hofu ya wayahudi. (Yohana 19:38-39) 🤫✝️
Yusufu wa Arimathaya alikuwa mtu tajiri sana na mwenye heshima kubwa. Aliandaa kaburi jipya, ambalo hakuwahi kulazwa mtu yeyote kaburi hilo lilichongwa kwenye mwamba. (Mathayo 27:57-60) Hili kaburi lilikuwa limeandaliwa kwa ajili yake mwenyewe, lakini kwa uaminifu wake na heshima kwa Yesu, aliamua kutoa kaburi lake mwenyewe kwa ajili ya Bwana. 🪦💔
Wayahudi wa wakati huo walikuwa na utaratibu wa kujiandalia makaburi yao kabla ya kufa. Hii ilikuwa ishara ya maandalizi ya mwisho na heshima kwa maisha. Makaburi haya yaliandaliwa kwa uangalifu sana mengine yaliwekwa kwenye miamba, na mengine yalichongwa kwa gharama kubwa. Kwa hiyo Yusufu kutoa kaburi lake mwenyewe ni tendo la kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa. 🏔️💎
Nicodemus, ambaye awali alimjia Yesu usiku kuuliza maswali kuhusu kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3), sasa anajitokeza hadharani kwa ujasiri mkubwa. Alileta mchanganyiko wa manemane na uudi wenye uzito wa ratli mia moja (karibu kilo 34) kiasi kikubwa sana cha manukato kilichotumika kwenye mazishi ya kifalme! (Yohana 19:39) 👑🌸
Kisha wakamchukua mwili wa Yesu, wakaufunga kwa sanda safi ya kitani pamoja na manukato kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi kuzika. (Yohana 19:40)
Sanda safi ya kitani ilikuwa nguo maalumu, ya heshima na usafi mkubwa, iliyotumika kuvikia miili ya watu waliokufa, hasa watu wa heshima. Kitani kilitokana na mmea wa flax na kilionekana kama vazi la kifahari hivyo, Yesu alizikwa kwa heshima kubwa licha ya kufa kama mhalifu. 🧣⚱️
Hii ni simulizi ya upendo wa kweli na ujasiri wa kiroho. Wakati wanafunzi wengine walikuwa wamejificha kwa hofu, Yusufu na Nicodemus walinyanyuka kwa ujasiri na kujitokeza hadharani kumheshimu Bwana. Ni fundisho kubwa kwetu leo kwamba wakati mwingine imani ya kweli inaonekana kwenye majira ya giza na maumivu unapojitokeza unapohitajika zaidi. 🌑✨
Pia, kaburi walilomzika Yesu lilikuwa karibu na mahali aliposulibiwa, katika bustani. (Yohana 19:41-42) Hii ina maana kuwa maandalizi yote yalifanyika kwa haraka kutokana na maandalizi ya sabato, lakini pia kwa makusudi ya Mungu kwa sababu kaburi hilo lilitarajiwa kuwa sehemu ya ushuhuda mkubwa wa ufufuo! 🌄🕊️
YESU ALIZIKWA KWA HESHIMA, LAKINI ALIFUFUKA KWA USHINDI! Halleluya! 🔥⛪
Fuatilia mafundisho zaidi ya kina kama haya kwa kulike na kufollow ukurasa huu wa Boanerges Evangelism Ministry. Usikose nafasi yako ya kukua kiroho na kufundishwa NENO la kweli la Mungu! 📖❤️✅