Wafanya biashara kugoma Jijini Mbeya

Wafanya biashara kugoma Jijini Mbeya

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Posts
3,019
Reaction score
579
Nimepata habari kutoka Mbeya kwamba wafanya biashara Jijini humo wamefunga maduka yao kuonyesha mgomo halisia, jana na leo hata wafanya biashara wadogo walio waoga wamegoma mpaka wakubwa waridhie. Kuna nini huko walioko Jijini Mbeya tujuzeni. Ama ndio vita ya TRA? maana TRA mkoa wa Mbeya na wilaya zake ni ubabe ubabe tu hapendwi mtu. Wana bei mbaya mno na ni wakatili kupindukia kwa sababu niliambiwa siku moja na mmoja wao kwamba wamepangiwa malengo ya kukusanuya ambapo wilaya yako isipofikia malengo hayo basi bosi wa TRA wilaya hiyo jihesabie kula nyasi. Unakusanya laki mbili kwa mwezi unaambiwa lipa laki moja unusu kodi, bado kodi ya nyumba na bili kadhaa na malipo ya posho kwa wafanyakazi. Niliwahi kufungua kijiwe nikalazima kufunga maana hawaelewi. Nilijikuta natoa pesa mfukoni kutoka kwenye mshahara wa kazini kwangu kila mwezi kununua bidhaa za kuuza, kulipa wafanyakazi, kulipa kodi kibao na leseni lukuki na michango ya hovyo ya lazima......Nikasema hapa mbeya sio business friendly bora nitafakari upya.
 
Back
Top Bottom