Wafanya biashara wa Dar wako shapu kuliko wa mikoani

Wafanya biashara wa Dar wako shapu kuliko wa mikoani

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Unaweza kukuta mfanyabiashara ana account nzuri mtandaoni, kama social media na google business lakini ukimtumia ujumbe kuulizia huduma au bei ya bidhaa, hakujibu. Mwingine anakujibu baada ya siku mbili na mwingine week ni mwendo wa blue tick. Majibu kujibiwa ni kama unatafuta hesabu za hiza utt ili uzielewe.

Wengine wanaajiri wafanyakazi lakini hawawafundishi kuhusu bidhaa na huduma wanazouza. Ukimuuliza mfanyakazi bei au maelezo ya huduma, anakuambia, “Ngoja nimuulize boss au boss hayupo mpaka harudi.” yaani hata ukifika ofisini na kumkosa boss, hakuna anayeweza kukuhudumia.

Inafika hatua unajiuliza baadhi ya watoa huduma wenye hixo account ni wenye biashara? au madali, sababu unapowafuata wanashindwa kukupa majibu sahihi kwa wakati. unauza bidhaa au kutoa hufuma usiyokiwa nayo au usiyotoa au unayotegemea jibu la mwingine.

Hii ndiyo hali ya biashara mikoani, kuna tofauti kati ya wafanyabiashara wa Dar es Salaam na wale wa mikoani katika kuhudumia wateja hii ni kwa asilimia 90, Tz nzima.
 
Sasa umeshasema Dar.

Akili yako ikiwa imepooza unakufa njaa.

Mda wote kichwa kinatakiwa kifanye kazi.
 
Back
Top Bottom