Wafanya biashara wabongo baadhi magumashi sana

Wafanya biashara wabongo baadhi magumashi sana

Marshmello

Member
Joined
Sep 16, 2018
Posts
86
Reaction score
131
Habari wana JF wote

Wafanya biashara wabongo baadhi magumashi sana hasa hawa madalali na wachuuzi wa bidhaa kutoka nje China, dubai nk wanazingua sana,

Sijui ni elimu ndogo niliyokuwa nayo au ushamba wangu tu

Anapost biashara yake kwenye mitandao ya kijamii kama fb, Instagram au TikTok katika ile bidhaa anayoiuza katika mtandao haandiki bei ' price tag'. Sio kesi, shida inakuja pale unamuibukia sehemu ya maoni ( comment section ) au dm unamuuliza bei mwingine anakupa namba ya simu ya whatsapp, mwingine anakupa location japo biashara yake kaipost online tatizo ni yule ambaye HAJIBU kabisa dm wala comment.

Anaposti mfano simu kwenye kurasa yake maelezo kibaoo mara hii simu kameli kali, processor sijui ram kubwa ila bei hakuna kwenye comment hajibu.

Mtu anauza mapazia mwenge amepost kwenye mtandaoni unamuuliza bei anakupa location ya duka lake "njoo dukani kwetu" unatoka zako mbagala au gongo la mboto mpaka mwenge unafika hapo dukani kwake anakwambia "ooh sorry this item was sold out".

Bora wale ukiwauliza bei wanakupa namba ya simu unajua kabisa hapa naenda kupigwa na kitu kizito kama sio kuuziwa kwa bei ya juu ' overprice" basi naenda kutapeliwa kabisa.

Wengine wananunua mashamba wanakata viwanja hasa nje kidogo ya mji na sehemu zilizopoa. Wanaauza kiwanja kwa bei mtamanisho kabisa ila vipimo vya kiwaki.

Utasikia

Viwanja kibaha kwa mathias

Bei milioni moja na laki 2

Ukubwa 20×20

Kwa akili ya haraka haraka unajua icho kipimo ni mita na wameandika hivyo labda kwa sababu wabongo wengi hawana elimu ya vipimo kwahiyo kwenye akili unajiseti kama ukubwa utakuwa sqm 400 hivi.

Lahaula!! Unafika site unakuta kakiwanja kadogo kama pool table unauliza vipi wanakwambia bosi kipimo ni miguu sio mita ila unaweza ukaunganisha hata vinne
 
Wengine wanapost bidhaa kwa bei rahisi kumbe ni bei ya china ukijichanganya ukawapa hela wakuletee unakutana na makato ya tra utatamani ungenunua kariakoo
 
Kutaja figure imekua Kazi, wenzutu bidhaa wanaweka na figure unaiona kama hutaki acha.
 
Back
Top Bottom