Wafanya biashara wenzangu, tupeane uzoefu wa ku-deal na wateja wa online

Wafanya biashara wenzangu, tupeane uzoefu wa ku-deal na wateja wa online

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Nimeona niwashirikishe hili kwa sababu naamini wafanyabiashara wengi humu wana experience kubwa ambayo inaweza kutusaidia wengine.

Mimi nafanya biashara ya vifaa vya ujenzi. Kwa kuwa siku hizi soko kubwa limehamia online, nilitengeneza page kwa ajili ya kutangaza bidhaa zangu. Kwa kweli nimekuwa nikishangazwa na response; napata wateja wengi zaidi kuliko nilivyotarajia.

Changamoto yangu kubwa ni kwamba duka langu bado ni dogo, hivyo siwezi kuwa na kila kitu dukani. Mteja wa online akihitaji bidhaa ambayo sina, mara nyingi nalazimika kuichukua kwa maduka mengine halafu nampelekea yeye.

Hapo ndipo nimegundua kwamba online business ina challenges zake ambazo huwezi kuziona mpaka uanze ku-deal na customers moja kwa moja.

Mfano, kuna mteja anasema anataka aje dukani, aone mzigo kwanza ndipo alipie. Mwingine anataka mzigo ufike kwake haraka sana, wakati wewe mwenyewe huna hiyo bidhaa na bado unategemea duka jingine likupe mzigo.

Kuna wakati unalipia bidhaa kwa supplier, unamtumia mteja, lakini akishapokea anasema “sijaridhika, siichukui” au anakataa kulipa. Mwisho wa siku wewe ndiye unabaki na mzigo ambao haukuwa hata kwenye stock yako.

Na changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya maduka unayonunua hayakubali return baada ya wewe kulipia na kuchukua mzigo. Hivyo mteja akikataa, risk yote inabaki kwako.

Pia kuna wateja wanaouliza bei kwa watu wengi online, wanakufanya uwatumie quotation, picha na details za bidhaa, halafu mwisho wanapotea bila hata kusema “sitachukua.”

Wengine wanaweza kukuwekea order, ukaiandaa na hata ukamlipia supplier, halafu dakika za mwisho wanabadilisha mawazo.

Kuna wanaotaka delivery ya bure, wengine wanataka kulipa baada ya mzigo kufika, na wengine wanataka mzigo ufike ndani ya muda ambao kiuhalisia ni mgumu kuutekeleza.

Sasa swali langu kwa wafanyabiashara wenzangu ni hili:

Ni changamoto gani kubwa mmekutana nazo katika ku-deal na online customers, na mmejifunza nini kutokana na hizo changamoto?

Na zaidi ya hapo, mmeweka mfumo gani wa kujilinda ili customer asikuachie hasara?

Mfano, mnachukua advance? Mna-confirm order kwa simu? Mnaweka terms za return? Mna-charge delivery kabla? Au mnawaamini tu customers?

Tupiane uzoefu hapa. Mafundi, wafanyabiashara wa bidhaa, online sellers, wholesalers na retailers – changamoto zenu na solutions mlizopata zitasaidia wengi.
 
Back
Top Bottom