mchapafito
JF-Expert Member
- Oct 16, 2013
- 608
- 301
Wasalaam wana JF,
Kwanza niwasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kazi iendelee!!!!), ndugu yenu nimekuwa nikipita kusoma comments kwa muda mrefu sasa, sijafungua uzi takribani miaka 8 sasa, lakini kama kichwa kinavyo jinasibu hapo juu imenibidi,
Hii barabara ya Kinondoni, ukiwa umetokea Morocco, ukishavuka mataa yanayoenda mwananyamala (karibu na babu Ally takeaway) hadi pale kwenye junction inayoenda Kinondoni makaburini, kuna akina mama/dada wanafanya usafi asubuhi
Concern yangu ni zile koni/VLC wanazoweka kama vizuizi barabarani kwa usalama wao, kwanza wanaviweka vibaya, pasi na utaratibu pia wanaweka maeneo hatarishi, just imagine mtu katoka kukimbia yellow light anakata kona tu anakutana na koni au dada wa usafi
Jamani, najua watu wa jiji mnapita humu, naomba muangalie hilo, atakuja tokea kichaa afanye mambo ya kutisha jamani, juzi hapo kuna kijana na Subaru Impreza almanusra amvunje miguu dada wa usafi pale kona ya Kinondoni Manyanya
Nawasilisha,
Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Mchapafito