Wafanyabiashara 650 waomba kufunga biashara TRA

Wafanyabiashara 650 waomba kufunga biashara TRA

Huyo anachapaje kazi analalamikiwa na wafanyabiashara yeye ka leader anatakiwa kuwa problem solver, ka anachapa kazi kwanini watu wengi wafunge biashara?
Sio anakomoa,
Kwa taarifa yako kule Moshi hadi wafanyakazi wa TRA hawapumziki,Hizo ndizo faida za kuwa na watu wachapa kazi na wanaomjua Mungu.

Kule Maofisa wanapiga kazi kwel kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gabriel alisema TRA kuanzia leo itafanya uhakiki maduka na biashara zote zilizoombewa kufungwa, na kwamba kama mfanyabiashara atabainika kuomba kufunga biashara yake huku akiendelea na biashara, mamlaka hiyo itawaburuza mahakamani na kuwatoza faini.
MAONI YANGU. HUU SIO WAKATI WA T.R.A KUWASHIKIA CHINI WANANCHI. BADALA YAKE WAKAE CHINI NA WAFANYA BIASHARA HAO AU HATA WOTE KUPITIA WAWAKILISHI THEN WAKUBALIANE JINSI WATAKAVYOWAFANYIA WEPESI, HIYO ITASAIDIA WATU KUENDELEA NA BIASHARA HUKU MAPATO YAKIWA YANAPATIKANA JAPO KIDOGO KIDOGO KATIKA WAKATI HUU WA JANGA LA KORONA. KULIKO KUTUMIA RUNGU NZITO ITAKAYOPELEKEA WATU KUJIFICHA NYUMBANI NA KUFUNGA BIASHARA KWA 100% KWANI IKITOKEA HIVYO MKOA NA TAIFA KWA UJUMLA LITAPOTEZA FEDHA NYINGI BILA SABABU ZA MSINGI.
OVER
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, imepokea zaidi ya maombi 650 kutoka kwa wafanyabiashara wakiomba kufunga biashara za maduka na hoteli za kitalii kutokana sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu walizozieleza ni watalii kusitisha safari zao za kuja kutalii na kupanda Mlima Kilimanjaro.

Meneja wa TRA, Mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari, na kuongeza kuwa licha ya maombi ya wafanyabiashara hao, TRA imekusanya zadi ya Sh. bilioni kumi sawa na asilimia 85 ya makisio yake kwa mwezi Machi mwaka huu.

Alisema TRA kila siku kuanzia mwezi Januari mwaka huu imekuwa ikipokea wastani wa barua za maombi zaidi ya 30 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara wakiomba kusimamisha biashara zao kwa muda, wengine moja kwa moja kutokana na mwenendo wa biashara zao.

Pia alisema tushio la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu corona, nao ukichangia kwa kiasi kikubwa.

Gabriel alisema TRA kuanzia leo itafanya uhakiki maduka na biashara zote zilizoombewa kufungwa, na kwamba kama mfanyabiashara atabainika kuomba kufunga biashara yake huku akiendelea na biashara, mamlaka hiyo itawaburuza mahakamani na kuwatoza faini.

Alisema kuanzia leo maofisa wa TRA watazunguka mitaani kukagua biashara zilizozofungwa na kila mfanyabiashara atapaswa kuonyesha mali zilizobakia na endapo kutakuwapo na ulaghai, mamlaka hiyo itawaburuza mahakamani.

Alisema Machi mwaka huu, TRA ilikusanya zadi ya asilimia 85 ya makisio ya makusanyo ya mapato, na kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya wafanyabiashara mkoani hapa kuwa na mwamko wa kulipa kodi kutokana na elimu na mahusiano mazuri kati ya wafanyabiashara na watumishi wa mamlaka hiyo.

Alisema kwa siku mbili mfululizo Machi 30 na 31 mwaka huu, watumishi wa TRA mjini Moshi walikaa ofisini hadi saa nne za usiku wakiendelea kutoa huduma kwa wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi kulipa kodi kabla ya Machi 31 kumalizika.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kujitokeza tarehe za mwisho za ulipaji wa kodi ili kuepuka kutozwa faini kwani hali hiyo inasababisha msongamano wa walipakodi na kiwakwamisha watumishi wa mamlaka hiyo kutoa huduma bora.

Gabriel alisema ili kuepuka misongamano isiyokuwa na ulazima na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona katika ofisi za TRA na benki, wafanyabiashara hawanabudi kujenga utamaduni wa kulipa kodi kabla ya tarehe za mwisho.

Alisema TRA mkoani hapa imeendesha kampeni ya utoaji elimu na faida za ulipaji kodi na wafanyabiashara kuwa na mwamko wa kulipa kodi.

Gabriel alisema tishio la corona limesababisha kusitishwa kwa safari za watalii kuja kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea hifadhi wanyamapori, hivyo kuathiri biashara ya utalii kwani hata hoteli za kitalii zimepunguza ama kuwaondoa wafanyakazi wanaotoa huduma kwa wageni wa utalii.

Alisema amefanya ukaguzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kubaini hakuna ndege yoyote kutoka mataifa ya nje wanaokuja kufanya utalii isipokuwa ndege zinaotoa huduma za kusafirisha abiria wa ndani.

NIPASHE
MODS Rekebisha kichwa isomeke "Wafanyabiashara 650 Mkoa wa Kilimanjaro...."
 
Kuna weekends 4 kila mwezi x3 sawa na siku 12.
Note; wastani 30 kwa siku
"Alisema TRA kila siku kuanzia mwezi Januari mwaka huu imekuwa ikipokea wastani wa barua za maombi zaidi ya 30 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara wakiomba kusimamisha biashara zao"

Januar, feb na march = siku 90
90×30= 2,700 ya maombi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi haka kamji kalivyo kadogo ni biashara gani sasa itabaki[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Tujiandae kisaikolojia anguko la kiuchumi linalokuja miezi 6 mbele tutatafutana.
 
Huyu Meneja wa TRA Moshi analaumiwa sana na Wafabyabiashara wengi. Amechangia watu kufilisika hasa wa maduka yaliyopo karibu kabisa na stendi ya mabasi makubwa na ile ya hais za KCMC.

Pia ana vitisho na fine mbaya za kulipisha watu kodi kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote TRA wanalenga kukusanya zaidi, so wanavyosema wamekusanya 85% ya malengo yao despite ya izo biashara zilizofungwa ni mafanikio makubwa
Despite biashara zilizofungwa... ni mafaniko makubwa.

Akili za kimaskini hizi!
 
Back
Top Bottom