DOKEZO Wafanyabiashara Busega walalamikia kuchangishwa kwa shuruti mchango wa mwenge

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Wafanyabiashara katika Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, wamelalamikia kile walichokieleza kuwa ni michango ya lazima kwa ajili ya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru, wakidai kuwa wanatozwa fedha kupitia maelekezo kutoka kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya bila mashauriano wala ridhaa yao.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia usalama na biashara zao, baadhi ya wafanyabiashara walidai kuwa maofisa kutoka ofisi ya wilaya na baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitembelea maduka yao kwa kutoa vitisho vya kufunga biashara iwapo hawatatoa michango hiyo.
Screenshot 2025-08-03 163142.jpg

​
====
Mdau mwingine kuhusiana na suala hili
​
Mimi ni Mkazi wa Mtaa wa Masanza Kona hapa Wilayani Busega, kuna changamoto ambayo imetokea jana na leo (Julai 31 na Agosti 1, 2025), kuna baadhi ya Watu wanafika mtaani na kututaka tutoe fedha wakidai ni kuchangia Ukimbizaji wa Mwenge.

Wanafika wakiwa na karatasi flani ambayo imesainiwa na mtu ambaye wao wanadai ni Mkuu wa Wilaya ya Busega, kwamba wakusanye michango kwa Wananchi.

Wanatumia lugha ya kutulazimisha na kututisha kuwa ambaye hatachangia atapelekwa Polisi, tumeenda kwa Viongozi wa Mtaa nao hawatupi majibu ya kueleweka.

Nimelazimika kuandika hapa JF ili ujumbe ufike kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Mwenge kwamba kama ni kweli au uongozo, kwani kama ni kweli utaratibu wanaotumia pia sio mzuri na unatuumiza kwa kuwa wanalazimisha watu.

Kibaya zaidi wanazunguka hadi kwa Wafanyabiashara wadogo ambao mtaji wao ni mdogo, wanachukua kiasi chochote wanachokikuta, mimi wamechukua kwangu Shilingi 500 wengine 10,000 yaani hatuna amani, na hapa wamesema watarudi kesho.
 
Bado
Watasombwa mpaka na malory kwenda kujaza uwanja
Unachangia kitu ambacho kina bajeti yake
 
Mnagoma changia mwenge ila octoba mnasema mnatiki changieni tu
 
Wafanyabiashara katika Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, wamelalamikia kile walichokieleza kuwa ni michango ya lazima kwa ajili ya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru, wakidai kuwa wanatozwa fedha kupitia maelekezo kutoka kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya bila mashauriano wala ridhaa yao.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia usalama na biashara zao, baadhi ya wafanyabiashara walidai kuwa maofisa kutoka ofisi ya wilaya na baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitembelea maduka yao kwa kutoa vitisho vya kufunga biashara iwapo hawatatoa michango hiyo.

View attachment 3427310
Haya yameanza upya. Kati ya manufaa makubwa yaliyo ondolewa na ujio wa vyama vingi ni michango ya mwenge, ulazima wa kufunga biashara kwenda kupokea viongozi na kwenye mikutano ya siasa. Ambalo limedumu japo lilipunguzwa makali na mh Mipango ni la misafara mirefu ya magari ziara za viongozi, na kufunga barabara mikoani wakati kiongozi hajapanda ndege Dar.
 
Ni kweli ,nimeona na mashuleni walimu wanalazimishwa kuchangia sh 5000,binafsi naona huu ni uhuni,kwani huu mwenge hauna bajeti au ni upigaji mwingine,

Nashauri watu wagome kutoa,hakuna cha kukufanya ukikataa kutoa
 
Kila mwaka watu wamekua wakichangishwa kwa ajili ya mwenge hali ya maisha mitaani ni ngumu sana kwanini wasiweke bajet kabisa ya huo mwenge
 
Back
Top Bottom