Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Mimi ni Mkazi wa Mtaa wa Masanza Kona hapa Wilayani Busega, kuna changamoto ambayo imetokea jana na leo (Julai 31 na Agosti 1, 2025), kuna baadhi ya Watu wanafika mtaani na kututaka tutoe fedha wakidai ni kuchangia Ukimbizaji wa Mwenge.
Wanafika wakiwa na karatasi flani ambayo imesainiwa na mtu ambaye wao wanadai ni Mkuu wa Wilaya ya Busega, kwamba wakusanye michango kwa Wananchi.
Wanatumia lugha ya kutulazimisha na kututisha kuwa ambaye hatachangia atapelekwa Polisi, tumeenda kwa Viongozi wa Mtaa nao hawatupi majibu ya kueleweka.
Nimelazimika kuandika hapa JF ili ujumbe ufike kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Mwenge kwamba kama ni kweli au uongozo, kwani kama ni kweli utaratibu wanaotumia pia sio mzuri na unatuumiza kwa kuwa wanalazimisha watu.
Kibaya zaidi wanazunguka hadi kwa Wafanyabiashara wadogo ambao mtaji wao ni mdogo, wanachukua kiasi chochote wanachokikuta, mimi wamechukua kwangu Shilingi 500 wengine 10,000 yaani hatuna amani, na hapa wamesema watarudi kesho.
Haya yameanza upya. Kati ya manufaa makubwa yaliyo ondolewa na ujio wa vyama vingi ni michango ya mwenge, ulazima wa kufunga biashara kwenda kupokea viongozi na kwenye mikutano ya siasa. Ambalo limedumu japo lilipunguzwa makali na mh Mipango ni la misafara mirefu ya magari ziara za viongozi, na kufunga barabara mikoani wakati kiongozi hajapanda ndege Dar.Wafanyabiashara katika Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, wamelalamikia kile walichokieleza kuwa ni michango ya lazima kwa ajili ya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru, wakidai kuwa wanatozwa fedha kupitia maelekezo kutoka kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya bila mashauriano wala ridhaa yao.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia usalama na biashara zao, baadhi ya wafanyabiashara walidai kuwa maofisa kutoka ofisi ya wilaya na baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitembelea maduka yao kwa kutoa vitisho vya kufunga biashara iwapo hawatatoa michango hiyo.
View attachment 3427310