Wafanyabiashara jifunzeni kuwa na kauli nzuri kwa wateja

Agrey998

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2019
Posts
417
Reaction score
550
Leo katika harakati zangu nimeingia kwenye moneyshop moja ndogo tu Arusha shida yangu ilikuwa ni kufanya miamala kadhaa, nimeingia nikakuta jamaa anapanga vitu nimefika pale hakuna cha karibu wala nini , ananiangalia AF kakunja sura nikauliza huduma ninayotaka hakujibu nikaona kaingia ndani basi nikamsubiri atoke , ametoka anauliza wewe una shida gani unanisimamia nje hapa, sikutaka kuongea zaidi nikaondoka.

Nimeenda kwingine nakuta jamaa anachati na simu tu namuuliza huduma ananiuliza ebu sema shida yako chap . Hapo pia nikaona hizi dharau nikaamua kwenda benki tu . Benki wamenuhudumia vizuri sana.

Wafanyabishara mtambue tu kitu kimoja kauli kwa wateja ni muhimu sana katika kumtunza mteja na kumfanya arudi siku nyingine hii itakusaidia sana hata kupandisha mauzo , kwa hao walionihudumia vibaya leo sidhani kama nitakuja kukanyaga tena kwenye biashara zao . Na msijidanganye kubwa mna wateja wengi tambueni kuna mtu ana ushawishi mkubwa anaweza akapeleka kundi kubwa la wateja au kuhamisha kundi kubwa la wateja kutoka kwako.

Na kingine pia ni kwamba hasira za nyumbani au mahali pengine usiziweke kwenye biashara yako , wateja wako ndio wanaokufanya wewe ukae pale wao wakuletee hela na Wewe uwape huduma nzuri utakuwa mwendawazimu kama utamnunia mtu anayekuletea pesa.

Jifunzeni kumsikiliza kila mtu na kutambua anataka nini msidharau wateja hata akiwa namna gani msikilize muhudumie kwa heshima akiridhika kesho atakuletea wengine au atakuwa mteja wa kudumu.

Nawasilisha
 
Wafanya biashara wa Arusha some percent kauli nzuri kwa mteja hawana… tena wale wa sokoni akuone unachagua chagua sana, au ubonyezee parachichi 😂😂 Anakushushua bila aibu
 
Hizo tabia ni reflection za background zao,hawawezi kubadilika labda wawe wana act tu kwakujilazimisha,

Customer care ni tatizo kubwa sana sehemu nyingi tu,na hili tatizo huenda likawa linachangiwa na malezi ya muhusika katika makuzi yake tangu akiwa mtoto.
 
Mimi nilikuwa najiona ndio mwenye matatizo kwa ku-demand good customer care kumbe nawe umo.

Napenda mtu akujali kama mteja siyo kwamba unamuulizia kitu ambacho kwa bahati mbaya hana au ameishiwa, muuzaji anakaa kimya akihudumia wengine au angalia simu kwa hata dakika 3 ndio anasema "SINA"
 
Kama ilikuwa ni jioni msamehe tu kwa kweli, mara nyingi jioni tunakuwa tumechoka sana au tumevurugwa na mwenendo wa biashara wa siku nzima
 
Leo katika harakati zangu nimeingia kwenye moneyshop moja ndogo tu Arusha shida yangu ilikuwa ni kufanya miamala kadhaa, nimeingia nikakuta jamaa anapanga vitu nimefika pale hakuna cha karibu wala nini , ananiangalia AF kakunja sura nikauliza huduma ninayotaka hakujibu nikaona kaingia ndani basi nikamsubiri atoke , ametoka anauliza wewe una shida gani unanisimamia nje hapa, sikutaka kuongea zaidi nikaondoka.

Nimeenda kwingine nakuta jamaa anachati na simu tu namuuliza huduma ananiuliza ebu sema shida yako chap . Hapo pia nikaona hizi dharau nikaamua kwenda benki tu . Benki wamenuhudumia vizuri sana.

Wafanyabishara mtambue tu kitu kimoja kauli kwa wateja ni muhimu sana katika kumtunza mteja na kumfanya arudi siku nyingine hii itakusaidia sana hata kupandisha mauzo , kwa hao walionihudumia vibaya leo sidhani kama nitakuja kukanyaga tena kwenye biashara zao . Na msijidanganye kubwa mna wateja wengi tambueni kuna mtu ana ushawishi mkubwa anaweza akapeleka kundi kubwa la wateja au kuhamisha kundi kubwa la wateja kutoka kwako.

Na kingine pia ni kwamba hasira za nyumbani au mahali pengine usiziweke kwenye biashara yako , wateja wako ndio wanaokufanya wewe ukae pale wao wakuletee hela na Wewe uwape huduma nzuri utakuwa mwendawazimu kama utamnunia mtu anayekuletea pesa.

Jifunzeni kumsikiliza kila mtu na kutambua anataka nini msidharau wateja hata akiwa namna gani msikilize muhudumie kwa heshima akiridhika kesho atakuletea wengine au atakuwa mteja wa kudumu.

Nawasilisha
Hii tabia ipo sana kwenye biashara nyingi hapa Arusha
Yani utafikiri mtu kalazimishwa
 
Mwanadamu hata umpe/umfanyie nini, haridhiki!

Ila tutaufanyia kazi ushauri wako.
 
Mi nilienda kwa mamantilie nikaagiza supu,nilipomaliza nikampa mhudumu 10,000( mwanamke),aisee alitolea kauli mbovu eti hivi una akili kweli unatoa 10,000 asubuhi hii yote,mijitu mingine sijui ipoje,nikamwambia lete niombe chenchi pale,inaonekana ule mtaa wanamnyima chenchi kwa kauli zake mbovu, baada ya miezi miwili anatafuta chumba cha kupanga na ule mtaa hamna vyumba kabisa,akaja anabembeleza nikamwambia unanikumbuka?mtu mwenye kauli chafu siwezi kumpangishia tutakosana tu,akondoka kwa aibu.
 
Leo katika harakati zangu nimeingia kwenye moneyshop moja ndogo tu Arusha shida yangu ilikuwa ni kufanya miamala kadhaa, nimeingia nikakuta jamaa anapanga vitu nimefika pale hakuna cha karibu wala nini , ananiangalia AF kakunja sura nikauliza huduma ninayotaka hakujibu nikaona kaingia ndani basi nikamsubiri atoke , ametoka anauliza wewe una shida gani unanisimamia nje hapa, sikutaka kuongea zaidi nikaondoka.

Nimeenda kwingine nakuta jamaa anachati na simu tu namuuliza huduma ananiuliza ebu sema shida yako chap . Hapo pia nikaona hizi dharau nikaamua kwenda benki tu . Benki wamenuhudumia vizuri sana.

Wafanyabishara mtambue tu kitu kimoja kauli kwa wateja ni muhimu sana katika kumtunza mteja na kumfanya arudi siku nyingine hii itakusaidia sana hata kupandisha mauzo , kwa hao walionihudumia vibaya leo sidhani kama nitakuja kukanyaga tena kwenye biashara zao . Na msijidanganye kubwa mna wateja wengi tambueni kuna mtu ana ushawishi mkubwa anaweza akapeleka kundi kubwa la wateja au kuhamisha kundi kubwa la wateja kutoka kwako.

Na kingine pia ni kwamba hasira za nyumbani au mahali pengine usiziweke kwenye biashara yako , wateja wako ndio wanaokufanya wewe ukae pale wao wakuletee hela na Wewe uwape huduma nzuri utakuwa mwendawazimu kama utamnunia mtu anayekuletea pesa.

Jifunzeni kumsikiliza kila mtu na kutambua anataka nini msidharau wateja hata akiwa namna gani msikilize muhudumie kwa heshima akiridhika kesho atakuletea wengine au atakuwa mteja wa kudumu.

Nawasilisha
Ukita huduma au kauli nzuri kwa wahudumu wa sehemu za biashara Bongo utakwama. (nikiri hata mimi nakwazika sana na huwa siendi sehemu zanye huduma mbovu). Ajabu ni kuwa watanzania wenyewe walishazoea na kukubali kunyanyaswa.
 
Hapana ni kwa sababu tuna shida ndio maana tunaenda tu hizo sehemu.
 
Na nchi nyingine zenye huduma nzuri hawana shida? Tunaenda kwa sababu ni utamaduni ambao tumeshaukubali. Tungekuwa tunawasusia na kwenda kwa wale wachache wenye huduma nzuri wangebadilika. BTW unapoenda dukani wewe mteja huna shida bali unataka bidhaa. Ukijiona una shida ndiyo mwanzo wa kukubali huduma mbovu.
 
Mimi nimewahi kunyang'anywa bidhaa niliyotaka kununua ikarudishwa kwenye shelfu, nikafurumshwa kutoka ndani ya duka kwa maneno ya kejeli tena kwa sauti kubwa "wewe una hela ya kununua hiki kitu wewe..? wa kununua uwe wewe? hebu toka apa..!" nikatolewa nje mkuku mkuku hadi wapita njia wakawa wananishangaa..

Kikubwa nilichojifunza, wafanyabiashara wengi hua "wanaokoteza" vijana tu na kuwaajiri mradi wanajua kupokea hela na kurudisha chenji. Hawa vijana/mabinti wanakua hawana uchungu wowote na biashara ilimradi mwisho wa mwezi mshahara wao unaingia. Wao huona wateja kama ni kero kwao na hawajali kama mteja atarudi au asirudi haiwahusu.
 
Wafanya biashara wa Arusha some percent kauli nzuri kwa mteja hawana… tena wale wa sokoni akuone unachagua chagua sana, au ubonyezee parachichi [emoji23][emoji23]
Anakushushua bila aibu
Nini Arusha, Nenda Kusini Mtwara na Lindi ni shida, hawamjali mteja na hawamwogopi hata kdg, mshkaji wangu mmoja alikwenda Lindi mjini akafikia maeneo ya karibu na stendi, akahitaji kunyoa akaenda jirani kuna bonge ya salon, milango iko wazi, muziki mkubwa na hakuna mtu, akaingia akakaa weee hakuna mtu akaenda jirani kuuliza wakamwambia yupo around angojee kdg, akaamua kutoka mitaa kama miwili akakuta watu wanacheza pool table, akawasalimia akauliza kama kuna salon jirani, wakamjibu huko ulikotoka kuna salon, akasema ni kweli ila kinyozi hayupo, wakamwambia kinyozi si ndio huyu tunacheza naye pool table!! Alichoka jamaa akaondoka zake, ndio wabongo walivyo.
 
Alafu utawakuta Vijana huko face book wanavyoomba kazi na kutia huruma, unakuta Kijana kaandika "naomba kazi saluni najua kunyoa, nina uzoefu" mtafute umpe kazi sasa ndio huyo anatekeza ofisi anashinda kwenye pool table.
 
Mimi wakati nasimamia kibanda cha kuingiza miziki na muvi nilikua najitahidi kua rafiki kwa mteja matokeo yake stori zikasambaa kwamba natongoza wateja.

Bro akanitimua akamuweka best yake. Ofisi ikachechemea kwakua muvi na miziki ni huduma ipo kila mahali so ukimjeuria mtu kukutema siyo tatizo.

Bro akaniplease nirudi by the time narudi nikakuta kafunga ofisi imekufa. Kuna frame ipo maeneo ya Kopa kwa anayetaka
 
Ujinga na Umasikini ndio Mama wa haya yote...hata kama unamuona Mtu smart lakini anatafunwa na background ya malezi ya Ujinga na Umasikini yanayozalisha stress za kudumu.

Wiki chache zilizopita nilikuwa maeneo ya Kisutu, nikahitaji huduma ya Kutoa pesa, ilikuwa Jpili au Sikukuu nadhani, Mji ulikuwa umetulia...nikaona bango kwenye chocho moja nikajongea..wakati naingia nikaona Jamaa Watatu wameketi wanaangalia kitu kwenye Simu aliyoishika mmoja wao...nikawasalimia nikawapita kuingia kwenye chumba...sikuona Mtu najaribu kuita ndio anakuja mmoja wa aliyekuwa pale nje, anasema "karibu" nikashtuka, sikutaka kuanzisha mjadala nikamwambia nataka kutoa pesa kwa crdb.akanijibu haraka haraka "hiyo sina nenda hapo chini"..akiwa palepale nje, kana kwamba akili yake yote ilikuwa kurudi pale nje alipokuwa na Wenzake.

Nikaondoka huku nikijisemea kuwa ingekuwa ni mimi ningetoa machaguo ya huduma nyingine...ambapo hata mimi nilikuwa tayari kutumia huduma nyingine lakini kwa vile niliona yeye hajali nikaondoka zangu.
 
Wafanya biashara wa Arusha some percent kauli nzuri kwa mteja hawana… tena wale wa sokoni akuone unachagua chagua sana, au ubonyezee parachichi [emoji23][emoji23]
Anakushushua bila aibu
AF mambo yakiwaendea kombo wanajua kutia huruma kweli na kukimbilia kwenye maombi wakati wanajiloga kwa kauli zao mbaya kwa wateja na majivuno yasio na maana.
 
Back
Top Bottom