Nini Arusha, Nenda Kusini Mtwara na Lindi ni shida, hawamjali mteja na hawamwogopi hata kdg, mshkaji wangu mmoja alikwenda Lindi mjini akafikia maeneo ya karibu na stendi, akahitaji kunyoa akaenda jirani kuna bonge ya salon, milango iko wazi, muziki mkubwa na hakuna mtu, akaingia akakaa weee hakuna mtu akaenda jirani kuuliza wakamwambia yupo around angojee kdg, akaamua kutoka mitaa kama miwili akakuta watu wanacheza pool table, akawasalimia akauliza kama kuna salon jirani, wakamjibu huko ulikotoka kuna salon, akasema ni kweli ila kinyozi hayupo, wakamwambia kinyozi si ndio huyu tunacheza naye pool table!! Alichoka jamaa akaondoka zake, ndio wabongo walivyo.