Wafanyabiashara jueni hii kero na kuwa huwa mnafukuza wateja.

Wafanyabiashara jueni hii kero na kuwa huwa mnafukuza wateja.

Ni kweli ni kweli. Nipo nafanya kazi sehem basi mabest wa boss wanavyojazana hadi natoka sijaingiza kitu ukiwauliza wateja ambao ni wanafunzi kwa kiwango kikubwa wananiambia tunawaogopa wale wababa. Nishaongea sana lakini cha mtu chake tafuta chako uwe mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia kama hizi ni kielelezo cha malezi mabaya mtu aliyoyapata na pia kutokuthamini muda.

Mtu aliyepata malezi mazuri na mwenye kuheshimu muda wake hata siku moja huwez mkuta amekaa kizembe zembe hivyo ktk ofisi za watu.
Ukikaa working shop ya msela omba hata umsadie vikazi kazi basi, sio kuwa kama mteja vile halafu hauna unachofanya unajaza nafasi tu.
Mfano kama ni barber shop omba hata ushike mashine mara moja kujifunza, sio kuvyoosha miguu kwenye sofa la ofisi ya watu umeshika na rimoti ya tv kama kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona mtu anaganda sana sehemu yako ya biashara, we mshikishe fagio tu (tumia lugha nzuri ya kishkaji " Oi mwanangu, chukua fagio basi rekebisha rekebisha kidogo si unajua tena usafi muhimu") , siku ya pili akirudi mshikishe tambara la deki (tumia lugha nzuri pia). Hapa taratibu ataanza kupaona pachungu na kesho yake hatorudi tena chenzi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya maduka utakuta wamejaa vijana wengi wanapiga soga,hii inawaondolea baadhi ya watu confidence ya kwenda dukani. Very bad for business life,ukikosa wateja unasingizia uchawi.Kuna saluni unakuta pia wapiga soga wanajibalaguza kwenye makochi huku wameshikilia remote za king'amuzi,huku wakikejeli chogo au nundu ya mteja anayenyolewa.
 
mkuu hii njia nzuri.. Asiee nimecheka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha nenda saloon classic na manunuzi anza kufanya maeneo yasiyo ya uswazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu saluni ninazosemea ni classic pia. Mara ya mwisho nimevyoa makambako Dama International salon (kwa wanaoifahamu watasema) ni classic ila shida wadada wa scrub na kuosha kichwa wanajaza mabest zao mle.

Juzi kati nikawa bagamoyo ndani ya mgahawa wa Dizz (classic as usual) namaliza kula sioni wa kumpa hela kumbe yupo kakaa nje anapiga stori na mshkaji wake.

Sikutaka kutoa mifano hai, ila hiyo miwili inatosha kuonesha kuwa hizo tabia zipo hata sehemu ambazo mtu hutegemei kuzikuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya maduka utakuta wamejaa vijana wengi wanapiga soga,hii inawaondolea baadhi ya watu confidence ya kwenda dukani. Very bad for business life,ukikosa wateja unasingizia uchawi.Kuna saluni unakuta pia wapiga soga wanajibalaguza kwenye makochi huku wameshikilia remote za king'amuzi,huku wakikejeli chogo au nundu ya mteja anayenyolewa.
Ukitoka tu hapo wanaanza kukunanga. Jamaa anaringa halafu bichwa baya kinoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, hiyo ni kero kubwa sana kwa wateja wengi. Sometimes unakuta mteja anaweza kuingia mahari kwa biashara, ila akajikuta anashindwa hata kununua au kuomba huduma fulani kwa sababu anaofia kuchorwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom