Wafanyabiashara Kariakoo: Jengo lililoanguka Kariakoo halikubeba tani 850. Hii inamaanisha Rais alipewa taarifa zisizo sahihi?

Matusi ni silaha ya wajinga, jitahidi uelimike uweze kupingana kwa hoja bila kutukana.
Lazima uambiwe ukweli wewe ni kichwa maji!
Concrete za gorofa hiyo unaona kabisa zilikuwa na uwezo wa kubeba tani 850?
Au na wewe ni chawa kila kinachofanyika kwa vile kimefanyika na kukubalika na Rais basi kiko sawa!
Usiwe msomi elimika na acha ujinga!
 
🚮🚮🚮
 
Kweli mpaka tani 850 za marobota ya pamba zienee kwenye kajumba hako sio mchezo.
 
We unapigia hesabu korosho!?..sisi wafanyakazi wa mchina hufuata mzigo wa tshet na sendo bandarini na kenta haitoshi kubeba,na hapo tumepanga flow moja, tshet 200 ni zaidi ya kilo 50
 
Mi kwa taarifa yako cjawah kuajiriwa. Ila nakusaidia. Gorofa moja la floor 8 lote linaweza kubeba Tani kumi. Hakuna nyumba hata moja mchina ana floor zaid ya 3. Wanachofanya wana magodown nje ya mji na store floor moja.
Unabisha nini wewe!?..mi natafuta ugali kwa mchina kila siku hapo msimbazi
 
Sielewi nini maana ya hili, wakimpa taarifa sahihi za uzito wa mzigo, inabadilisha nini kwenye taarifa ya rais, au Jengo litasimama? Au mtu kaidai Bima?
 
Tani moja =kilo 1000. Sasa inawezekana kabisa zilikuwepo zaidi ya hata kilo 850 mana jengo lilikuwa limejaa mizigo
 
Mi kwa taarifa yako cjawah kuajiriwa. Ila nakusaidia. Gorofa moja la floor 8 lote linaweza kubeba Tani kumi. Hakuna nyumba hata moja mchina ana floor zaid ya 3. Wanachofanya wana magodown nje ya mji na store floor moja.
uongo mtakatifu, ghorofa 8 tani 10? acheni utani, nyumba tu za kupanga zinazidi hio tani 10 furniture za watu sembuse stoo za bidhaa.

kukupigia tu hesabu rahisi

ghorofa 8 kila ghorofa apartment 2 ni apartment 16

kilo 10,000 gawanya 16 ni around kilo 600 kila nyumba, uzito tu wa binadamu 5 ama 6 wanaoishi nyumba moja unazidi kilo 300 eka vitanda, kabati, na vikorokoro vingine unakuta tani kadhaa.
 
Reactions: Cyb
Niambie jengo gani lina tan 10 ya mzigo wa mchina maana mi nawajua wachina wote wenye mastoo za mizigo kkoo mi pia nafanyabiashara kkoo. Sema ni yupi mwenye rani kumi kama hatujakukamata kwa uongo hapa.
boss kontena moja ni zaidi ya tani 20, njoo kkoo usiku uone watu wanavyoshusha kontena, kuclaim hakuna mchina mwenye tani 10 ni kusema kkoo hakuna mchina anayeleta kontena ambayo ni hoja ya kipuuzi sana.

achana na tani 10, kuna wachina wana hadi tani 100 kwenye store za frame tu, juzi kati kuna mchina wamemuibia mzigo wa 60m kwenye store ya duka ambao ni zaidi ya kontena (tani 20) na hajajua hapo hapo hadi alipokuja kupiga hesabu.
 
Taarifa ilisema hivi "Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema katika zoezi la uokoaji wa jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo mwezi Novemba, imebainika jengo hilo lilikuwa limebeba takriban robota 2,040 na viroba 10,051 vya nguo zilizokadiriwa kuwa na uzito wa tani 850 licha ya jengo hilo kuwa na uwezo wa kubeba tani 250 pekee." Kwa wataalamu tupigieni mchanganuo
 
Kimsingi na kiuhalisia, Jengo lile halikuwa na uwezo wa kubeba mizigo mkubwa wenye uzito huo wa tani 850, completely impossible.
 
Kwani hiyo tofauti ya uzito inabadili nini ikiwa jengo limeanguka na kuleta madhara makubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…