D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,399
- 3,666
Wafanyabiashara wa kariakoo ni wahuni sana usije ukajichanganya kuwaamini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani Ili iwe tani,tunategemea uzito au ujazo shekhe🙄🙄Kukaa kimya sio solution, tani hata 2000 zinaweza kuingizwa kwenye hilo jengo...inategemea na uzito wa mizigo sio ujazo.
Ila huo nao ni ukweli pia!!!Wafanyabiashara wa kariakoo ni wahuni sana usije ukajichanganya kuwaamini
Taarifa inasema tani 850 za mizigo sio na jengo.Kwani uzani wa jengo lenyewe hauhesabiwi kwenye uzito wa jumla?
Mahesabu yenu haya ya magumashi mnayajua wenyewe.Taarifa inasema tani 850 za mizigo sio na jengo.
Lile jengo mmewahi litumia kabla halijaporomoka?
Kama hamjawahi mnaweza fanya makadirio kwa majengo yanayokaribiana nalo almost yako sawa yote ni majengo machovu nguzo nyembamba na yamechoka hali ya hewa. Hata majengo ya pembeni nayo pia hayana uwezo wa kubeba mzigo wa tani 850.
Hii report inashindwa kuwataja wamiliki waliokuwa wanachokonoa foundation ya nyumba, viongozi waliotoa vibali vya ujenzi, injinia au fundi uchwara. Vyote hivyo inashindwa inakuja kutoa taarifa za kubumba ili ionekane walioangukiwa na vifusi ndio wenye makosa kuweka mizigo mingi.
Elezea kwa ufupi tani 1000 zinabebwa na makasha mangapi na yenye ukubwa gani?Kwa msongamano huo wa bidhaa, hata wangesema tani 1000 bado ingeweza kuwa sawa!View attachment 3225049
Hukumuelewa raisi,mama alimaanisha mzigo au bidhaa zilizokuwa ndani ya jengo zilikuwa na uzito wa tani 800.Mzigo wa jengo ni jengo lenyewe, sio mzigo kutokea nje ya jengo.
Hao wafanya biashara waache kujifanya ni ma engineer.
Kwa matumizi ya baadaye.Kwani hiyo tofauti ya uzito inabadili nini ikiwa jengo limeanguka na kuleta madhara makubwa.
Ushakamatwa uongo, LolIli nikupe machimbo siyo!?
Ya mzigo gani? Steel ama nguo? Hayo mafurushi hata yangekuwa kontena 200 hayawezi kukupa tani hizo 850Mimi pia mfanyabiashara nimewahi weka container 8 nusu floor, ghorofa 3 yenye basement inaingia zaidi ya container 40 hasa kwa viwanja vya kkoo ambavyo ni vikubwa.
Tiles, Container 200 ni zaidi ya Tani 4000 nyie Jamaa hizo hesabu mnapiga vipi? Mfanyabiashara huwa haachi kilo zake ovyo ovyo, kama bidhaa ni nyepesi atatumia 40 feet ili mzigo uwe mwingi zaidi.Ya mzigo gani? Steel ama nguo? Hayo mafurushi hata yangekuwa kontena 200 hayawezi kukupa tani hizo 850
Twenty fit Nina hadi Bill of landing kama unataka ushahid container 8 za tiles nimezisimamia mwenyewe container hadi container zote 8 zinaingia stoo, na kila container inazidi tani 20.Sio kweli niambie eneo gani wewe. Acha uongo. Conteiner gan lina tan 20 linashuka kkoo. Lina mzigo gan. Ni ft fit ao twenty fit.
Tuchukulie at minimum hio 250 SQM ni roughly 7500 sqft na kila sqft jengo la raia inabeba kilo 18 standard za ujenzi so kila floor Tani 135, jengo la Ghorofa 3 ground na basement Lina floor 5 jumla Tani 6751. Sijajua uliposema hasa kwa viwanja vya kkoo ambavyo ni vikubwa umelinganisha na viwanja vya wapi. Maana viwanja vya kkoo vinarange kati ya sqm 250 mpaka 350sqm.
2. Payload capacity ya container ya futi 40 baada ya kutoa uzito wa container lenyewe ni takriban tani 27. kwa tani 850 hapo tunazungumzia takriban container 32 za futi 40. Je zinaweza kuingia kwenye hilo jengo au lah, hilo siwezi jua kwa sababu sijui ukubwa wa jengo ulikuwaje.
3. Hata kama hizo container 40 zimeweza kuingia kwenye hilo jengo, bado kuna swali linafuata. Hayo macontainer yalikuwa na bidhaa gani? Maana aliyepakia viatu, aliyepakia mipira, aliyepakia vipuri na aliyepakia mchanga kila mmoja kwenye container la futi 40 uzito wao hautokuwa sawa kutokana na spacing ya bidhaa ndani ya container.
4. Bidhaa zinazouzwa kwenye lile jengo zinajulikana nyingi zikiwa ni viatu na nguo sio vitu vizito kama vile spare. Ili kufikia uzito wa tani 850 hapa hatutozungumzia tena container 32. Zinaweza fika hata 50. tuchukulie kila floor amekodi mtu mmoja. ina maana kila mtu atakuwa amehifadhi container takriban 16 za futi 40. Kwa wafanyabiashara wengi kuagiza container 16 kwa muda mmoja ni wachache sana tena kwa mbinde. Wengi utaskia wameagiza container 5 na labda 5 nyingine zipo njiani.
Na huyu naye pia kadanganya. Kariakoo kuna majengo mengi ya ghorofa 10 na yote ni magodown matupu. Je yanaweza kuhimili uzito wa mizigo yote hiyo?
Hapo sasa swali litarudi kwa wahandisi wa serikali waliotoa vibali vya ramani za ujenzi. Kama ujenzi ulifuata utaratibu mfano kwa maghala ya kuhifadhia vitu vizito ni 125 psf, reinforcement imekidhi viwango basi hamna tatizo.
Ama sasa kama ramani ilipitishwa kwa kwa matumizi ya makazi ambayo 40psf mpaka 50 zinatosha, halafu baadae watu wakajichukulia maamuzi ya kubadilisha matumizi na kugeuza store, Hicho sasa ni kimbembe kingine.
Hiki kitofali umemrushia nani kwa hio Bibi au?Jengo lina floor tatu libebe tani 850 hivi uko na akili kweli au umejaza usaha kichwani huko!
Kibali Cha Ukarabati maana yake Nini katika muktadha wa Ujenzi?Nadhani ni kibali cha ukarabati kwani hilo jengo ni la zamani. Kama kulikuwa na kibali
Yaani ilibeba kontena zaidi ya 28 za tani 30 si mchezo. Halafu hizo tani ziwe za nguo mnaweka hadi juu ya paaTani 850 unazijua ndugu!!??
Mimi mfanyabiashara wa ufuta na korosho ukiniambia jengo lile lilikuwa limebeba tani 850 siwezi kukuelewa!