Wafanyabiashara Kariakoo: Jengo lililoanguka Kariakoo halikubeba tani 850. Hii inamaanisha Rais alipewa taarifa zisizo sahihi?

Kwani uzani wa jengo lenyewe hauhesabiwi kwenye uzito wa jumla?
Taarifa inasema tani 850 za mizigo sio na jengo.

Lile jengo mmewahi litumia kabla halijaporomoka?
Kama hamjawahi mnaweza fanya makadirio kwa majengo yanayokaribiana nalo almost yako sawa yote ni majengo machovu nguzo nyembamba na yamechoka hali ya hewa. Hata majengo ya pembeni nayo pia hayana uwezo wa kubeba mzigo wa tani 850.

Hii report inashindwa kuwataja wamiliki waliokuwa wanachokonoa foundation ya nyumba, viongozi waliotoa vibali vya ujenzi, injinia au fundi uchwara. Vyote hivyo inashindwa inakuja kutoa taarifa za kubumba ili ionekane walioangukiwa na vifusi ndio wenye makosa kuweka mizigo mingi.
 
Mzigo wa jengo ni jengo lenyewe, sio mzigo kutokea nje ya jengo.

Hao wafanya biashara waache kujifanya ni ma engineer.
 
Mahesabu yenu haya ya magumashi mnayajua wenyewe.
Kwa mfano wa maelezo mtu ukisikia anasema gari 7t anamaanisha mizigo peke yake bila gari?
 
Mzigo wa jengo ni jengo lenyewe, sio mzigo kutokea nje ya jengo.

Hao wafanya biashara waache kujifanya ni ma engineer.
Hukumuelewa raisi,mama alimaanisha mzigo au bidhaa zilizokuwa ndani ya jengo zilikuwa na uzito wa tani 800.
 
Alafu kuna kajamaa kabishi humu kanaelekezwa badala ya kuelewa kenyewe kanatembeza dislikes tu itakua ndio kaandishi ka hizo tani 8500
 
Mimi pia mfanyabiashara nimewahi weka container 8 nusu floor, ghorofa 3 yenye basement inaingia zaidi ya container 40 hasa kwa viwanja vya kkoo ambavyo ni vikubwa.
Ya mzigo gani? Steel ama nguo? Hayo mafurushi hata yangekuwa kontena 200 hayawezi kukupa tani hizo 850
 
Ya mzigo gani? Steel ama nguo? Hayo mafurushi hata yangekuwa kontena 200 hayawezi kukupa tani hizo 850
Tiles, Container 200 ni zaidi ya Tani 4000 nyie Jamaa hizo hesabu mnapiga vipi? Mfanyabiashara huwa haachi kilo zake ovyo ovyo, kama bidhaa ni nyepesi atatumia 40 feet ili mzigo uwe mwingi zaidi.

Hata hizo nguo ushawahi kuona zikishushwa, njoo Swahili Mchikichi wanashusha CBM za boxer hapa uone, Binadamu habebi, zimekuwa pressed vibaya mno inabidi watu karibia 6 kusukuma then wanakata ndio wakinga wanagawana.
 
Sio kweli niambie eneo gani wewe. Acha uongo. Conteiner gan lina tan 20 linashuka kkoo. Lina mzigo gan. Ni ft fit ao twenty fit.
Twenty fit Nina hadi Bill of landing kama unataka ushahid container 8 za tiles nimezisimamia mwenyewe container hadi container zote 8 zinaingia stoo, na kila container inazidi tani 20.
 
Tuchukulie at minimum hio 250 SQM ni roughly 7500 sqft na kila sqft jengo la raia inabeba kilo 18 standard za ujenzi so kila floor Tani 135, jengo la Ghorofa 3 ground na basement Lina floor 5 jumla Tani 675

Tuchukulie 350 SQM ni roughly 10,500 sqft Kwa 18 kg ni Tani 189 Kwa jengo Tani 945.

So nyumba kkoo Ghorofa 3 na basement inabeba baina ya Tani 675-945

Hapa Tu tumemaliza hio case, jengo lilibeba mzigo mwingi zaidi uwezo wake maana ni zaidi ya Tani za Ukubwa WA Kiwanja.

Pia mkuu usifananishe Ukubwa WA bidhaa zikiwa Dukani na kwenye container ama stoo, bidhaa zinakua pressed hasa aina ya nguo, ushawahi fungua belo la mtumba, Shuka, jora la pazia etc, Wana pack na machine na kuzipress vibaya mno.
 
Nadhani ni kibali cha ukarabati kwani hilo jengo ni la zamani. Kama kulikuwa na kibali
Kibali Cha Ukarabati maana yake Nini katika muktadha wa Ujenzi?

Kibali Cha Ujenzi ni jina la ujumla kuelezea kuhusu Vibali vya kuweza kufanya maendelezo ya ujenzi, aidha kwa ujenzi mpya au kwa muendelezo wa kazi za zamani
 
Tani 850 unazijua ndugu!!??
Mimi mfanyabiashara wa ufuta na korosho ukiniambia jengo lile lilikuwa limebeba tani 850 siwezi kukuelewa!
Yaani ilibeba kontena zaidi ya 28 za tani 30 si mchezo. Halafu hizo tani ziwe za nguo mnaweka hadi juu ya paa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…