Wafanyabiashara kutoka Tanzania kufuata mizigo ya bei nafuu Uganda, imekaaje?

Titty, lakini inakuwaje sasa kwamba UG hawana bandari lakini bado wanafikisha mzigo hapa kwa bei nafuu kiasi kwamba wafanyabiashara wetu wanatoka Dar/Mza na kununua hapa; na wakifikisha TZ wanauza na kupata faida!! Something is not connecting well here. Kwa mantiki hii, ingebidi wafanyabiashara wa UG ndio waje TZ kununua mzigo.

Nimeelewa point yako; lakini hili la mzunguko wa mzigo hadi ufike Kampala na bado ukaweza kununuliwa kwa faida na Mfanyabiashara wa TZ limekaaje???
 
MODS, ASANTENI KWA KU - EDIT KICHWA CHA HABARI. NILIANDIKA NIKIWA NA HARAKA! YOU ARE DOING GREAT JOB GUYS...!! LONG LIVE JF.
 
Mkuu ni kuwa ukadiriaji wa kodi kwetu ni wa kukomoa kitu unanunua $10 wao wanasema $20 sasa ukilipa kodi kwa kiwango hicho lazima bei itapanda. Hakuna kuaminiana kati ya mwagizaji na tra.
I HOPE WATAWALA WETU WANAONA HILI...!!
 
Na mimi itabidi nikanunue huko unga
Unga pamoja na kutolipiwa kodi lakini wenyewe ndio unafuata kanuni za logistics kwa kuwa bei rahisi zaidi kwenye point of entry.hivyo huwezi pata bei rahisi kama tanzania
 
umeonaaa eeeee yaani kodi inakuwa kubwa kushinda bidhaa uliyonunua sasa hapo kuna nini cha ziada kama sio wanakutukomoa hawa serikali
.
Sasa kama ni suala la kodi kwetu kuwa kubwa, je ukiingiza hiyo mizigo Tz kutoka Uganda hulipi kodi?
 
Kodi inalipwa kama kawaida. Uganda wananunua nguo toka ulaya na bei ni nzuri. Wafanya biashara wengi Dar hununua nguo za bei ya China na quality ya chini. Wakifikisha Dar bei huwa haina tofauti na nguo toka ulaya kupitia Uganda ambayo qualify yake ipo juu mno.
 
Reactions: MC7
Wafanya biashara wengi hununua nguo za bei ya chini China na quality huwa chini. Wakifikisha mzigo Dar bei zao huwa juu sawa na nguo za quality ya juu toka ulaya kupitia Uganda na hatimaye Tanzania. Ushuru na kodi husika hulipwa mpakani kama kawaida. Nawapongeza TRA mipakani kwa kazi nzuri.
 
Vipi ukinunua gari Uganda ukija Tz unatozwa kodi kama ile ungetozwa bandarini?
 
Naomba exchange rate kati ya Uganda na Tz .......tsh :......ug sh

Kwa hiyo unashauri tununue magari uganda
 
Nipe exchange rate ya Uganda na tz
 
nauli kwenda na kurudi kutokea arusha ni tsh ngapi?
 
Tumefundishwa vibaya kudhibiti shughuri za Bandari zetu. Ushauri wao umetupeleka chaka, sawa bidhaa zinazopitia bandari za tanzania hazinunuliki kwa ukali wa bei, wafanyabiashar wote wanazikimbia. Wawe wa Tz au hata wale wa nchi za SADIC na COMESA.
Tutafakari udhibiti wetu na kustakabari wa shughuri zatu za kiuchumi.
 
Mani, hiyo concept ya Kodi kubwa inabidi kuifikiria zaidi.

Ukisema hivyo ina maana wafanya biashara wengi hawalipi Kodi wanapoingiza mzigo kuja Tanzania. Je hii ni kweli.
Sometimes kuwa soft kwenye ukusanyaji wa kodi kunasaidia kujenga uchumi wa nchi. Ndio maana jamaa alikuwa soft kwenye kukusanya kodi, lakini kila MTU alifurahia maisha. Huyu wa sasa yuko very tight ila kila MTU anachukia maisha. It is just a matter of strategies tu basi.
The same ndio ambayo inatumika na Uganda, ambayo pia hutumika mpakani MUTUKULA.
Kwepesha kodi ili maisha(multiplically) yaendelee
 
Ni walaini kwenye masuala ya ukusanyaji wa kodi, jambo ambalo linaruhusiwa kiuchumi ni kiforodha. Watu wa forodha wao wanatakiwa wafacilitate trade na sio kuwa chanzo cha kujusanya kodi. Kuwa Laini kwenye kukusanya kodi za kiforodha ili maisha yaendelee.
 
Naomba exchange rate kati ya Uganda na Tz .......tsh :......ug sh

Kwa hiyo unashauri tununue magari uganda
Kanunue toka kwenye bonded warehouses ambazo bado hazijasajiriwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…