Wanajamvi,
Hapa Niko katika kituo cha Bus liitwalo FRIENDS jijini Kampala nikielekea nyumbani Tz. Ninachokiona hapa na wafanyabiashara wa KiTz toka Dar na Mwanza wamefungasha mizigo ya nguo, viatu, na vifaa vya MAGARI kuvileta Tz.
Najiuliza inakuwaje Uganda haina bandari lakini bado mizigo yao inapitia Bandari ya Dar na Mombasa lakini bado vitu ni being nafuu kiasi kwamba watanzania wanavifuata huku??
Naomba wanauchumi mlioko hapa mtuelewesha Tz kuna tatizo gani? Hii bandari ya Dar, Tanga na nyinginezo zinatunufaishaje??