Wafanyabiashara Makanjanja wamewagharimu sana Wafanyabishara waaminifu, hivi sasa wanatumia nguvu nyingi kumshawishi mteja

Wafanyabiashara Makanjanja wamewagharimu sana Wafanyabishara waaminifu, hivi sasa wanatumia nguvu nyingi kumshawishi mteja

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!

Wafanyabishara na wachuuzi ambao kwa muda mrefu wamekuwa si waaminifu wamewagharimu wafanyabishara waaminifu kiasi kwamba wanapata taabu sana kuwashawishi wateja ambao walishakosa imani!

1. WAUZA MACHUNGWA SEGERA

Hapa kuna wahuni wao ulikuwa ukifika eidha unatoka Mkoani unakuja Dar es Salaam au unatoka Dar es salaam unaelekea mkoani na ukasema angalau uwabebee ndugu, jamaa, familia na marafiki matunda aina ya Machungwa, unalipa pesa lakini wao wanakuwekea machungwa mazima kwa juu na chini ya mfuko wanakujazia machungwa karibu yote mabovu au yameoza.

Wao kwa ujinga wao walidhani kuna mtu wanamkomoa kumbe walikuwa wanajikomoa wenyewe!,bahati nzuri mara nyingi wateja wa hizo njia huwa wanajirudia, hivyo wakawashitukia na machungwa yao yakawa yanawadodea.

Leo wanatumia nguvu nyingi kuwashawishi wateja lakini ni kama wamechelewa, UJINGA WAO UMEWAGHARIMU.

2. WAUZA ASALI

Hawa walijifanya wajanja kwa kuchanganya Asali na madude wanayoyajua wao wakidhani wanamkomoa mteja kumbe walikuwa wanajikomoa wao.

Leo wanatumia nguvu kubwa mno kuwaaminisha wateja namna ya kuifahamu asali fake na halisi ili angalau wateja wapate kununua mambo yao yaende, lakini ni kama wamechelewa kwasababu wateja wengi walipigwa mno kiasi kwamba hata hamu ya asali hawana.

Watanzania walikuwa walaji wakubwa wa asali lakini baada ya wafanyabiashara makanjanja kuwalaghai wateja,watanzania wengi wameamua kuwaangalia tu huku wakiendelea kuzurura na asali zao wakipigwa jua! UJINGA WAO UMEWAGHARIMU.

3. VITUNGU/VIAZI VINAVYOPANGWA KWENYE SADOLIN NJIANI

Hawa wanaendelea kuoga machozi ya ujinga wao. Abiria na wateja wengi walikuwa wakifika njiani wakikuta Viazi au Vitunguu vikiwa kwenye Sadolin wanamwambia mfanyabiashara awawekee haraka kwakuwa wao pia wanaharaka, wafanyabiashara hao makanjanja walikuwa wanatumia mwanya huo kuwaibia wateja/abiria wakidhani uenda walikuwa wakiwakomoa wateja kumbe walikuwa wakijidanganya!

Unakuta Sadolin katikati imechomelewa au imekatwa na ikapachikwa kopo, mteja anaponunua akidhani ni Sadolin nzima kumbe kapunjwa kwa kuwekewa bidhaa nusu! Abiria na wateja wengi hivi sasa walishawasanukia na wanawaangalia tu huku wakiendelea kudoda na bidhaa zao juani! Hivi sasa wanaula UJINGA WAO walioutengeneza wenyewe.

4. WAUZA MAZIWA FRESH KWENYE MAKOPO AU CHUPA ZA MAJI

Hawa nao walidhani kuna mtu wanamkomoa kumbe walikuwa wakijikomoa wenyewe. Kwenye chupa ya Lita 1 unaweza kuta maji ni ml 650 halafu ml 350 ndo ukakuta ni maziwa! Wao walikuwa wanapata faida ya mara mbili halafu hasara inabaki kwa mteja! Wateja baada ya kuligundua hilo wameona wawe wananunua maziwa ya kwenye Pakti tu kuliko utapeli wa hao jamaa.

Yawezekana leo wapo wanaouza maziwa halisi kabisa lakini kwakuwa hapo awali makanjanja waliwaharibia, imekuwa ngumu sana hivi sasa kuaminika tena kwa wateja na hivyo kutumia nguvu kubwa kuwaaminisha wateja!

5. WASAJILI LINE (FLEELANCERS)

Bahati nzuri na mimi nimewahi kupita huko,hivyo ninajua kwa kina namna madogo wanavyo hustle ili angalau wapate kamisheni nzuri. Mwanzo Hawa madogo walikuwa wanapiga sana kazi, lakini baada ya wajinga wachache kuwaibia wateja fedha kwenye akaunti zao za mitandao ya simu, hivi sasa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu mno ya kutokuaminika tena kutoka kwa wateja na kibaya sana hivi sasa wote wanaonekana ni makanjanja tu.

Mteja hivi sasa anaona ni heri aende umbali mrefu ofisi ilipo kuliko kusajiliwa na hao "Vishoka" ,japokuwa wapo waaminifu lakini waliharibiwa soko la wateja na wenzao ambao hawakuwa waaminifu.

Hivi sasa hata Kamisheni zao zimekuwa zi nzuri kwasababu wale wateja waliopaswa kuwasajilia lini mpya wanaona ni heri waelekee ofisini moja kwa moja! UJINGA WA WACHACHE UMEWAPONZA WENGI WAAMINIFU hivyo wanaendelea kusota wakitembea juani kama wehu huku hakuna wakuwaamini tena!

Poleni sana wafanyabiashara waaminifu, endeleeni kupambana!
 
Kuweni macho na wauza michanga na kokoto kwenye malori. Wamechomelea bati lingine kwenye malori kwa ndani kupunguza ujazo ulioonyeshwa wa k.m. 4 cubic metres kumbe ni 3 cubic metres wakati umelipia 4 cubic metres. Hata urefu wa nondo za kujengea siyo wenyewe na WMA hili wanalijua. Nondo zinakatwa kupunguza urefu lakini bei ni ya urefu kamili. Matatizo yapo kila mahali. Kuweni makini.
 
Uaminifu ni mtaji. Aliyenao, kamwe hawezi kosa mkono kwenda kinywani.

Kwenye ajira saizi Degree ni nyingi mno, hawapati ajira Si sababu hakuna ajira HAPANA,

Hawaajiriki sababu ya tamaa ya mafanikio ya haraka, anataka ndani ya mwaka mmoja ajenge nyumba yenye swimming pool na anunue Range.

Na hapo ndipo ulipo mzizi wa tatizo la ajira Kwa wasomi Hasa katika sekta binafsi.
 
Ujanja mwingi ambao Mtanzania huwa anajisifia,huwa ni upumbavu mfano mdogo ni hapo Tunduma,jinsi wajinga wachache walivyo haribu sifa ya Mtanzania Safi kwa Wazambia.

Uku niliko Wafanyabiashara kutoka DRC wanawafanya kitu mbaya makanjanja wa Watanzania kwa kuvunja uaminifu.
 
Kwenye asali wamezingua sana. Bora ununue tu supermarket. Pia kwenye nyama choma wanapunja balaa.
Nyama choma sio kutupunja tu Ila wanatuchanganyia na nyama ya mbwa. Unapokula nyama choma Mombo usiku uwe makini sana, Kuna wanaochanganya nyama ya mbwa na mbuzi, Sasa na ule ulevi na sifa wakati wa kusindikiza maiti usiku unajikuta unanunua nyama ya mbwa kwa Bei ya form six.

Lakini pia hivi vimishkaki Mbezi stendi ya daladala usiku kuwà makini Mara mbili, huwa wanachanya nyama ya walinzi na ya paka, Ile harufu ya kuvutia na vile viungo vinakufanya usigundue kwamba umekula nyama ya mlinzi.
Siku hizi mbwa Koko wameadimika maeneo ya Mbezi.
 
HAPA UMEPIGA MULEMULE!
 
Nimecheka eti nyama ya mlinzi
 
Wauzaji saruji(cement) kinafunguliwa kwenye kona kinapunguzwa kinabandikwa gundi na kimfuko laini cha nguo.
Wauza sukari jumla kiroba kinafunguliwa kinapunguzwa kinashonwa tena.

Hao wachawi hata kwetu 'Daslama' wapo.
 
Kila kitu kinachofaa kufungua, kupunguza na kufungwa tena hua inafanyika hiyo. Ukikuta sehemu wanauza cement ya kupima, sukari ya kupima nk ujue hiyo wanayopima wamepunguza kwenye mfuko.
 
Ile mishikaki ya Bei rahisi ni malapulapu(reject) yanauzwa machinjioni nenda ukajionee vingunguti au tegeta sio kuandika uongo tu hapa.
 
Wauzaji saruji(cement) kinafunguliwa kwenye kona kinapunguzwa kinabandikwa gundi na kimfuko laini cha nguo.
Wauza sukari jumla kiroba kinafunguliwa kinapunguzwa kinashonwa tena.

Hao wachawi hata kwetu 'Daslama' wapo.

Mi nadhani mfuko wa Cement na Sukari mkuu ukiwa kama mteja au mfanyabiashara wa rejareja si unatakiwa kuupima mfuko kabla ya kununua au huwa ni uaminifu tu ukidhani kweli ni Kg 50?
 
Mi nadhani mfuko wa Cement na Sukari mkuu ukiwa kama mteja au mfanyabiashara wa rejareja si unatakiwa kuupima mfuko kabla ya kununua au huwa ni uaminifu tu ukidhani kweli ni Kg 50?
Ukitaka mfuko mmoja au 10 uwahi ukajenge unapewa hakuna kupima utaambiwa unabishana na maandishi ya mzalishaji?
Hakuna anayepima mkuu.
 
Kila kitu kinachofaa kufungua, kupunguza na kufungwa tena hua inafanyika hiyo. Ukikuta sehemu wanauza cement ya kupima, sukari ya kupima nk ujue hiyo wanayopima wamepunguza kwenye mfuko.
Mbolea ya kupima...
Ingawa serikali inakataza Mbolea za kupimiana kienyeji kwa kilo.
 
Back
Top Bottom