Wafanyabiashara na Wasafirishaji wagoma Songea wakitaka kuonana na viongozi wa mkoa, DC Cosmas atoa saa 24

Wafanyabiashara na Wasafirishaji wagoma Songea wakitaka kuonana na viongozi wa mkoa, DC Cosmas atoa saa 24

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wafanyabiashara na wasafirishaji wa Songea mjini wamegoma wakitaka kukutana na viongozi wa mkoa ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Wafanyabiashara hao wamedai wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na mitaji yao inazidi kufa.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Songea ndugu Cosmas ameibuka na kutoa saa 24 wafanyabiashara hao wafungue maduka vinginevyo watapata tabu sana.

Nao LATRA wamefuti ruti ya mabasi yatokayo Songea mjini kwenda Mbinga kufuatia mgomo huo.

Chanzo: ITV habari.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii nchi ina viongozi wenye vibuli,wasiofikiri na kutoa maamuzi ya kukurupuka,kisa hawagaramiki na chochote maishani na mishahara minono wanapata pamoja na posho, wananchi hawasikilizwi zaidi ya kupewa amri tu migogoro na uonevu imekuwa sehemu ya maisha ya Mtanzania, sasa hivi siku ikipita bila makashikashi unashukuru Mungu,
Kazi ni moja tu , ni kuswaga kwa kwenda mbele hakuna kusikiliza kero hapa,
Ila walichosahau ni kuwa leo na kesho ni vitu viwili tofauti,
Kwa sababu cheo ni dhamana
 
DC hatujatumia busara kutoa masaa 24 kwa wadau wake muhimu.Haya mambo ya kupeana madaraka kwa ukada hizi ndio garama zake.
 
Tujulishe changamoto zao,ili tuwezekujua na kutoa michango ipasavyo.
Tatizo lilianza mapema mwezi Jana pale mamlaka zilipoamuru magari tote ya abiria yapakie na kushusha stendi kuu ilojengwa nje ya mji wa Songea (shule ya tanga)

Hii imepelekea maduka kuzunguka stendi ya mjini Kati kukosa wateja, stendi mdogo ya majengo pia imefungwa ikiwaacha wadau waliowekeza mitaji yao maeneo hayo bila wateja.

Hii kwanza ilipelekea nauli kupanda kwa baadhi ya maeneo kwakua umbali uliongezeka toka shule ya tanga Hadi maeneo husika mfano peramiho nauli ilipanda toka 1000 Hadi 2000

Leo wafanyabiashara wa maduka ya jumla, mafuta, pamoja na wale wanaosafirisha abiria ndani ya mkoa wametia mgomo kushinikiza utaratibu wa awali wa kupakia na kushusha ktk vituo vilivyofungwa.

Halimashauri inapoteza mapato kwa kuzuia shughuli ktk vituo hivi.

Wangeacha mabasi ya mikoani kupakia shule ya tanga na Seedfarm, lakini kwa ndani ya mkoa basi majengo, msamala, lizaboni na mjini Kati waendelee vilevile.
 
Sisi Wana peramiho tunateseka sana haijawah tokea naul ikapanda kwa 100% serikal haiangalii mitaji ya wafanyabiashara na mapato yatashuka sna katka manispaa sababu songea n mj mdogo sna wenye watu wachache ukivuruga utaratbu kidogo jua na biashara nying zitasimama
 
Tatizo lilianza mapema mwezi Jana pale mamlaka zilipoamuru magari tote ya abiria yapakie na kushusha stendi kuu ilojengwa nje ya mji wa Songea (shule ya tanga)

Hii imepelekea maduka kuzunguka stendi ya mjini Kati kukosa wateja, stendi mdogo ya majengo pia imefungwa ikiwaacha wadau waliowekeza mitaji yao maeneo hayo bila wateja.

Hii kwanza ilipelekea nauli kupanda kwa baadhi ya maeneo kwakua umbali uliongezeka toka shule ya tanga Hadi maeneo husika mfano peramiho nauli ilipanda toka 1000 Hadi 2000

Leo wafanyabiashara wa maduka ya jumla, mafuta, pamoja na wale wanaosafirisha abiria ndani ya mkoa wametia mgomo kushinikiza utaratibu wa awali wa kupakia na kushusha ktk vituo vilivyofungwa.

Halimashauri inapoteza mapato kwa kuzuia shughuli ktk vituo hivi.

Wangeacha mabasi ya mikoani kupakia shule ya tanga na Seedfarm, lakini kwa ndani ya mkoa basi majengo, msamala, lizaboni na mjini Kati waendelee vilevile.
Asante kwa ufafanuzi
 
Nao kwanini walimruka kiongozi wa wilaya wakaenda moja kwa moja mkoani?

Amandla...
 
Ina maana wao viongozi wanajifanya jeuri ngoja waje watumbuliwe
 
Back
Top Bottom