Wafanyabiashara Nchini Kunufaika na Biashara na Malipo ya Kimataifa

Wafanyabiashara Nchini Kunufaika na Biashara na Malipo ya Kimataifa

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
160
Reaction score
172
photo_2026-11-02_18-15-22.jpg
Wafanyabiashara na wajasiriamali wa Kitanzania wanatarajiwa kunufaika na biashara na malipo ya kimataifa kutoka mataifa zaidi ya 200 yenye uwezo wa fedha za kigeni zaidi ya 25 hatua ambayo inafungua fursa za biashara kimataifa .

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya Benki ya KCB na Kampuni ya Peypal na mkuu wa idara ya fedha na huduma za kidigitali kutoka KCB Josina Njambi ambaye amesema hatua hiyo ni katika kuwezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wanaotumia mitandao ya kidigitali kupata malipo ya kimataifa kutoka mataifa zaidi ya 200 ambapo mtandao wa Peypal unafanya kazi.
photo_2026-11-02_18-15-29.jpg

photo_2026-11-02_18-15-26.jpg
Kwa upande wake Priscus Kessy memeja mwandamizi huduma za kidigitali kutoka KCB amesisitiza ushirikiano huo ni kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na matumizi ya digitali ambayo kwa tanzania yamekuwa yakikua kwa kasi.

Bao baadhi ya wajasirimali wakizungumza wameshukuru kwa ushirikiano kwa kuwa utasaidia kutatua changamoto ya malipo ya fedha kimataifa.
 
Back
Top Bottom