Wafanyabiashara soko la Mbezi Beda wadai DC Kheri James anamhujumu RC Makalla kwa kuwarejesha baadhi yao kusikoruhusiwa

Wafanyabiashara soko la Mbezi Beda wadai DC Kheri James anamhujumu RC Makalla kwa kuwarejesha baadhi yao kusikoruhusiwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wafanyabiashara wadogo katika soko jipya la Mbezi Beda Ubungo wamemlaumu mkuu wao wa wilaya Kheri James kwa kuwarejesha baadhi ya wafanyaniashara maeneo yasiyo rasmi.

Wamedai kila wakimfata DC James ofisini kwake anawaambia wakaanxie kwanza kwa mchungaji kabla ya kwenda kwa askofu akimaanisha mchungaji ni Afisa Biashara na askofu ni yeye ( DC)

Wafanyabiashara hao wametafsiri vitendo vya DC James kama hujuma za makusudi dhidi ya agizo la mamlaka ya juu hivyo wamemuomba RC Makalla kuingilia kati kabla hali ya hewa haijachafuka hapo Ubungo wilayani.

Chanzo: ITV habari
 
Wafate ushauri wake, waanzie Kwa mchungaji
 
Kuna watu walibebwa na mwendazake kwa ajili tu ya kuwa ni wa ukaya. Kheri James anapaswa kusoma alama za wakati.
Labda hautaki u-DC.

Ujue kwa sasa yupo kundi moja na Lijualikali, Joshua Nassary na Mashinji!
 
Chanzo ITV habari alafu huna hata Video , Joni acha unafiki au upate hata uafisa tarafa[emoji1787]
 
Eti Anamhujumu Rc Makala
emoji38.png
Sasa tutasemaje wale waliorudi Kariakoo, Posta , Tandika hao madc amuwaoni ? Umelipwa sh ngap?
 
Huu ndio ukweli, DC amewaambiwa warudi wafanye biashara na kibaya sana sasa wanafunga hadi barabara na kufanya kuwepo na foleni muda wote.
Mzee Makala tembele eneo hili uone namna DC wako anavyohujumu juhudi zenu na Raisi Mama Samia ktk kuweka miji yetu ktk hali ya mpangilio.
 
Huu ndio ukweli, DC amewaambiwa warudi wafanye biashara na kibaya sana sasa wanafunga hadi barabara na kufanya kuwepo na foleni muda wote.
Mzee Makala tembele eneo hili uone namna DC wako anavyohujumu juhudi zenu na Raisi Mama Samia ktk kuweka miji yetu ktk hali ya mpangilio.

Mnataka watu wakale wap? acheni roho mbaya mbona amsemi atembelee kariakoo, Mbagala ambapo wamegoma kuondoka , Tegeta nk..

wewe machinga wa Mbagala una roho mbaya sana
 
Mama kiponda ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo maeneo ya mbezi amelalamika majibu ya mkuu wa wilaya alipotaka kujua kauli yake kuhusu kuwachanganya machinga sehemu za biashara walizopangiwa.

Source ITV taarifa za saa
 
Bwana James amesahu kiichofanya hadi yeye aletwe hapo? Ni kama vile mbinu inayotumia kumchomoa Jaji ni kumpa Ubalozi na badae kumtumbua huko huko aliko.Awe makini
 
Makalla ana kazi kuishi na huyu mdunda sindano za sumu
 
Heri James na Dotto James ni watoto wa Dada yake na Mwendazake.
Kuna watu walibebwa na mwendazake kwa ajili tu ya kuwa ni wa ukaya. Kheri James anapaswa kusoma alama za wakatil
 
Back
Top Bottom