hapa ndo ilipo tofauti ya Mkenya na Mtanganyika, wakati wewe unahimiza watu twende sasa wakenya walikuwa huku tangu hata hawajakubaliana kuhusu amani. Kuna opportunity nyingi saana na wakenya wanazishikilia karibu zote, ila ukumbuke kuna na challenge nyingi saana. mfano hawa wadinka wanafikiri wana haki ya kila kitu, ni kitu cha kawaida mtu kwenda hotelini anaagiza anachotaka na baadae anakataa kulipa ukiwauliza wanakumabia wanakula faida ya uhuru wao
pia kuna swala la sheria, jeshi na hata polisi hawakona displine kabisa ukitofautiana na polisi au mjeshi anawweza kukulima risasi mara moja, Pia kama unataka kuwekeza unatakiwa uwe na mbia kutoka south sudan, japo kiafrica hili sio issue kubwa
wakenya wengi wameajiriwa na mashirika ya misaada, wengine kampuni za kikenya kama KCB, na wanasaidiana kweli, wakenya wengine wamehamua kujinunulia maeneo makubwa saana ya Ardhi kwani huu udongo unarutuba kweli
Kwa watanzania badala ya kujenga hizi hoteli sinza na kwingineko wangeweza kuzijenga JUBA na wangerudisha pesa zao very soon. Tatizo la watanzania wengi tunaogopa kuchukua maamuzi magumu, na hatujishughulishi kusaka taarifa, ndo maana tunapitiwa na hizi opportunities. nimesikia CRDB wanataka kufungua tawi BURUNDI hawa jamaa wangeenda SOUTH sudan naamini wangepata faida kweli,kama KCB ya kenya inavyo vuna pesa huku,