Wafanyabiashara wa hizi bidhaa mjitafakari

Watu wanatajilika kiongozi.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hizi biashara zote zimetengeneza matajiri wakubwa sana. Kuna jamaa alijenga ghorofa kwa kuuza chupi za kike MUCCOBS moshi. Mzee Ruwaichi wa tabata TBL ililipia trip ya Marekani yeye na familia yake kwa kuongoza mauzo ya bia DSM. Pharmacy ina hela kuna kijana nilisoma naye ni Prof Norway ana pharmacy katika station tatu za SGR. Na ni biashara pekee aliyoshawishika kuwekeza nyumbani. Anasema ndio ambayo anaona faida inayoendana na hela anazoweka. Kwa hiyo issue ni kuhangaika na kutafuta wapi unapopaweza.
 
wewe ndio taahira

its not your job kupangia market demand yake

consumer yupo ndio anaamua nini kiuzwe au kisiuzwe sio wewe mbeba chumvi
 
Una roho ya kimaskini. Kauze mavi
 
Isingekuwa Dhambi
Ningeanzisha kiwanda cha kutengeneza spirit najua mwaka wangu mmoja tu ningetoboa
 
Isingekuwa Dhambi
Ningeanzisha kiwanda cha kutengeneza spirit najua mwaka wangu mmoja tu ningetoboa
Umeenda viwandani ? Hawatengenezi pombe, wanaagiza pure ethanol kutoka India wana-dilute na kuongeza flavour. Wana special machines kufanya dilution. Yaani ni dhambi kuliko aisee. kuna kiwanda cha pombe kali kipindi cha Corona kilikuwa kinazalisha sanitizer. Aisee jiulize mtu gani atapika pombe aichachishe mpaka apate Spirit kwa kupitia distilation halafu aitumie kutengeneza sanitizer. Watu wangu wanaunguza maini kwa kukosa maarifa. Hivi viwanda vyote vya pombe kali vilazimishwe kuonyesha uzalishaji wao.
 
Yes mkuu ndo spirit inapopatikana ndo mana nikasema isingekuwa Dhambi spirit ingenitoa
 
Kila mtu ana namna yake ya utafutaji kwani hao wanunuaji hawajui kama hizo pombe ni sumu, waache waendelee kuongeza pato la taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…