Wafanyabiashara wa Kigeni na hali halisi kwa Wazawa

Wafanyabiashara wa Kigeni na hali halisi kwa Wazawa

AfricaUnited

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2010
Posts
2,367
Reaction score
1,293
Kwa kipindi cha muda kama wa miezi miwili iliopita, nimekuwa niichunguza kwa umakini mwenendo wa Uchumi wetu Tanzania. Nimeshangaa sana kuona sehemu kubwa ya Uchumi unashikiliwa na makampuni makubwa ya kigeni na wale raia wa kutoka nje ambao wameomba uraia wa kuishi hapa,au wale ambao ni wageni na wamezaliwa na kukulia hapa Tanzania hasa Wahindi na Wachina.

Biashara nyingi zimetawaliwa na Wahindi, secta nyeti kabisa zimeshikiriwa na wageni, bidhaa nyingi zinazalishwa na wageni au wazawa wenye asili ya kihindi, kiarabu, au kichina; Hii pia imesababishwa na serikali kuuza Viwanda au kuingia ubia na makampuni makubwa kutoka nje.

Katika kipindi cha miaka ya 1960s - 2008s, makampuni mengi yaliyokuwa yanamilikiwa na serikali yaliuzwa kwa bei che kabisa kwa wageni na wazawa wenye asili ya kigeni. Na makampuni mengine na viwanda vilivyouzwa ni kutokana na serikali kukosa sera mbadala ya kuweza kuvisimamia na kudai kuwa hawana uwezo wa kifedha na rasilimali watu kuweza kuviendesha.

Nimeshangaa sana hata vikampuni vidogo kabisa vilikuwa vikiuzwa kwa bei ya chini kabisa wakati serikali ina uwezo kabisa wa kiviendesha. Je, Serikali inakosa hata hela za kukopa nje kuweza kuviendesha kweli, au ingeweza kuwahusisha wazawa kununua hisa kwa wingi, zaidi mambo yamekuwa ndivyo sivyo (NICOL).

1. Nilishangaa sana niliposikia mwekezaji mmoja toka nje akijisifu kuwa nchi fulani hivi ya Africa anaenjoy tax exemption na pia anapata wafanyakazi kwa bei ya chini kabisa zaidi ya mara KUMI ya anaowalipa China kwa wanaofanya kazi ile ile. Na kuna Kongamano moja la kimataifa Raisi alikuwa akiwaomba wawekezaji kuja wekeza Tanzania kwani kuna wafanyakazi wa bei rahisi na motisha nyinginezo. Hii imesababisasha pia wageni kuja huku na kulipa wazawa kiasi ambacho hata kwa matumizi kwa mwezi ni kidogo sana na ni kima cha chini cha kumlipa mtu.

2. Kuna Wahindi wanafanya biashara huwezi amini, hao wanaishi kwenye magorofa /apartment Kariakoo na wengine kwenye majumba ya kifahari hapa hapa kwenye nchi yetu, sasa sijajua zaidi kama serikali inatumia fursa hata hio kuweza kuwabana zaid kenye kodi au ndio yale ya kumbana Mtanzania masikini alipe kodi huku hao wafanyabiashara kubwa na wageni wakipewa misamaha au kukwepa kodi kiujanja na kizembe tu.

3. Serikali imekuwa ikilalamika kila siku kuwa walipakodi (TAX BASE ) ni ndogo. Je hao hao wachache wanaotakiwa kulipa kodi wanaliapa kikamilifu? Au ndio njia ya kumbana Mjasiriamali anaekuwa kwenye biashara.

4. Ni wakati sasa wa Watanzania kuangalia kiongozi atakaekuja maana yote haya yanatokea KWA AJILI YA UFISADI, Rasilimali za nchi zinatafunwa na wazawa kizembe tu. Pesa zinazoibiwa na mafisadi ni kiwango cha kutosha kujenga Zahanati, Shule na Maabara za kisasa tu.

5. Lipi la ziada serikali inalifanya kuhakikisha wazawa wanakuwa na direct access kwenye secta nyeti pia au kuweza kujiendesha wenyewe? Maana misaada haiwezi kuiendeleza nchi hata siku moja.

Kama mfano jirani yako anakusaidia hujiwezi kwa vitu vingi kama chakula, basi atakachokuwa anakwambia utakuwa unakubali tu. Anaweza sema hata kitu ambacho ni kinyume na maadili na kukudhalilisha sana. Nchi za nje wakija kutoa misaada kama kawa wanachukua Twiga kiulaini.


Tunakoelekea, bila Serikali kutumia njia mbadala, viwanda vyetu wazawa vitakuwa si chini ya kumi. Utandawazi na Uwekezaji toka nje si mbaya, bali kuangalia faida watakazozipata wazawa kupitia huo uwekezaji.

Na pia Serikali ikijipanga vizuri, basi inaweza fufua viwanda vilivyokuwa na kuviendeleza bila kuviuza kwa wageni.

Itaendelea wiki ijayo..

Yapi Maoni yako kuhusiana na haya?

Mdau,
Iringa, Tanzania.

 
Kwa foreigners kuja kufungua viwanda, biashara na hata bidhaa ambazo tunahitaji kwa wingi ni vizuri kwa nchi inayoendelea. Yaliopita yamepita sasa kila nchi inaangalia maslahi yake tu angalia Kenya leo wanatukataza kubeba watalii toka Nairobi hiyo ni kwa ajili ya maslahi yao mbele, kama hawa wanasiasa uchwara wanaoangalia maslahi yao zaidi badala ya utaifa kweli hatutafika.

Lakini mwekezaji kuwekeza kwetu ni ajira kwetu kama serikali ijayo itasimamia kodi kwa wawekezaji vizuri na sio kupanga mikakati mingi ambapo matokeo yake wakubwa wanaingia share na serikali kukosa mapato.
 
Back
Top Bottom