Kwan unafikir hawapendi kuacha hiyo Biashara ? Kam ulikuw hujui ngoja nikupe Elimu,... Hayo makundi yana Muunganiko wa matawi tofaut tofaut kam vile ilivyo kwenye siasa ambavyo kuna Muunganiko wa Nchi zinazounda NATO au BRICS,
basi na kwenye madawa ndo hivyo hivyo .... Na wenyew wana Makundi yao yanayounda umoja Husika
Hivyo inapotokea Umeanza kufanya hiyo biashara hat kam upo peke yako Wakikubaini tu hata kam Ulikuwa na Mzigo wa Kilo moja basi inabid Ujiunge na Kundi litakalokufata ujiunge nalo na ukikataa Kinachofata ni kifo,
Na ubaya unakuja kwamba ukishajiunga kwenye hayo makundi basi kuna katiba zao na moja ya masharti ni Hakuna mwanakundi anayetakiwa kujitoa au kuhama nchi bila ruhusa ya Mkuu wa Muungano,
Ikitokea umetaka kujitoa au Umehama nchi bila ruhusa bas kinachofata ni kifo tu na usijidanganye unawez ukajificha sehem yyte duniani maan hawa Jamaa wana mtandao mkubwa mno ambao unafika had kweny vyombo vya Usalama,
Hivyo unapokuwa umejipanga Kuanza hii biashara bas tambua kwamba hakuna kuludi nyuma kamwe,... Ni mwendo wa kusonga mbele tu mpaka Mauti itakapokufikia.