Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Licha ya wateja kulalamika kuhusu matapeli wa biashara mtandaoni lakini pia kuna wateja matapeli.
Kuna rafiki yangu ni mfanyabiashara Kariakoo sasa kuna siku akapata Delivery Kimara Temboni. Mteja akamwambia atalipia mzigo ukifika. Basi bwana boda akaja dukani kachukua mzigo kaelekea Kimara sasa akiwa njiani mteja akampigia boda akamuomba amnunulie umeme wa elfu 10 akifika atamrudishia. Basi boda akanunua umeme akamtumia.
Sasa boda kafika Kimara mteja hapokei simu ikabidi ampigie muuzaji na yeye akampigia mteja hapokei na simu ikazimwa. Boda kafika dukani ikabidi muuzaji amlipe gharama ya usafiri ila boda akawataka na ya umeme aisee ugomvi uliibuka pale mwenye duka anamwambia mimi sikukutuma umnunulie umeme.
Wateja na nyie muwe na huruma. Wewe kama mfanyabiashara ulishatapeliwa na mteja?