Wafanyabiashara wa Nairobi waandamana kuzuia Wafanyabiashara Wachina wadai wanaua biashara yao

Wafanyabiashara wa Nairobi waandamana kuzuia Wafanyabiashara Wachina wadai wanaua biashara yao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
China3.jpg

ef34848d-4b8f-41fb-ab4f-9c83fceef2cc.jpg

Maandamano yametokea Mitaa ya Dubois, Gikomba na Nyamakima Jijini Nairobi wahusika wakidai uwekezaji unaofanywa na Wafanyabiashara raia wa China kuuza vitu kwa bei ya chini ni hatari kwa biashara ya wazawa.

Wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti ikiwemo kudai 'Kuna uvamizi wa Wachina', wamefika hadi Ofisi ya Makamu wa Rais Rigathi Gachagua wakitoa ujumbe kuwa biashara zao zilindwe, ambapo Askari Polisi wamelazimika kuingilia kati na kutawanya waandamanaji.

Tukio hilo limetokea siku moja kabla ya Gachagua kukutana na wafanyabiashara wa kigeni kuzungumzia ongezeko la wageni hasa raia wa China na Pakistan wanaofanya biashara Nchini Kenya.

9c47c201-6a7d-445d-a31d-7a627aa7307b.jpg
China.jpg

China1.jpg

China2.jpg

China 4.jpg

=====================

Nairobi Traders Block Road Protesting Chinese Retailers, March to Gachagua Office

Traders from Nairobi's Dubois Street, Gikomba market and Nyamakima market took to the streets on Tuesday, February 28 to protest what they termed as the infiltration of Chinese retailers in the country.

The traders marched to the office of the Deputy President Rigathi Gachagua to demand protection for their businesses.

In a video seen by Kenyans.co.ke, the traders were carrying pluckards while blowing trumpets and whistles as they walked from downtown Nairobi to the central business district.

The protesting traders blocked Harambee Avenue just in front of the Deputy President's office as they sought for audience with the police.

Videos shared online show a police vehicle at the scene of the protests just in front of Gachagua's office.

The protests come just a day before the date of the planned meeting between the Deputy President and the traders aimed at addressing the rising number of foreign traders in the country, especially Chinese and Pakistani nationals.

This is after the DP gave in to pressure and scheduled a meeting with Nyamakima traders that is slated for Wednesday, March 1.

According to Importers and Small Traders Association Organizing Secretary Anne Nyokabi, the meeting will address foreigners' 'takeover' of local markets.

Among the issues to be discussed in the meeting include the demands by the local traders to be allowed to control the wholesale and retail ends of the value chain.

"We wanted to demonstrate against the government following serious infiltration of our business space by foreigners, especially from China and Pakistan," Nyokabi revealed in an interview on Inooro TV.

However, she indicated that word about the intended protests reached Gachagua who sent emissaries to the traders with the intention of a round-table meeting on March 1.

"There are those among us who are still meeting to plan to go ahead with planned street protest marches but I urge them to first embrace this window of dialogue," Nyokabi indicated.

The traders from various competing trade centres first took their complaints to Gachagua last week, appealing for action and threatening to stage protests.

During the first meeting, Gachagua reiterated that he will act as the guardian angel for Mt Kenya region-based business enterprises in Nairobi.

"President William Ruto’s government will respect businesses and will never entertain any aspect that undermines existing businesses" the Deputy President indicated.

Gachagua indicated that Nyamakima traders had suffered during former President Uhuru Kenyatta's regime and it was time that suffering comes to a stop.

However, some economic experts warn that this might defeat the global concept of liberalisation of trade and usher in pricing cartels.

The developments came in the wake of controversy elicited by the coming of China Square controversy that saw the popular mall at Unicity along Thika road closed indefinitely.

The retail outlet was indefinitely closed with the owner citing a number of reasons that they wanted to work on before reopening.

Trade Cabinet Secretary Moses Kuria announced government plans to push for the China Square closure only to on Sunday peddle backwards on the stand.

Source: Kenyans.co.ke & The-star.co.ke
 
Ndio walikua wanasema sisi Tanzania tunaogopa ushindani wa kibiashara, ila wao ni "aggressive" hawaogopi na nchi Yao Iko huru kwa yeyote kufanya biashara[emoji23][emoji23][emoji23]
Waoga sana hao afu wanajifanya aggressive[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]....
Sasa wangekutana na mtifuano wa wahindi,wapemba, wachagga na wakinga ka hapo kariakoo cjui wangefanya nn maana k.koo ya moto sio kitoto
 
Ndio walikua wanasema sisi Tanzania tunaogopa ushindani wa kibiashara, ila wao ni "aggressive" hawaogopi na nchi Yao Iko huru kwa yeyote kufanya biashara[emoji23][emoji23][emoji23]
Haujawasikia wakenya vizuri. Ni hivi
Wachina bidhaa zao wanauza bei nafuu zaidi kuliko wakenya. Mfano Radio wachina wanauza 200 lkn wabongo wanauza 800.
Wakipiga hesabu gharama ya mzigo kutoka china na hiyo bei ya 200 kwao ni hasara.
Hawana shida na wachina kuuza bidhaa ila ni bei. Wamesema km watauza km wao sawa ila km ni tofauti waondoke.
Soma vizuri. Nimesikiliza BBC swahili, tena wakenya walikuwa wanahojiwa
 
Wangetumia muda huu kubuni mbinu zaidi za kibiashara
Muwe mnaelewa kwanza habari kabla hujachangia kitu!!yaani mimi naenda china nanunua bidhaa kwa sh.100 bei ya jumla kiwandani, nakuja kenya naiuza kwa sh.1500!!huyo mchina analeta bidhaa hiyo hiyo na kuiza kwa sh.700!! Tena kwa reja reja!!hapo nitabuni mbinu gani ya biashara niweze kumshinda huyu mtu!!!
 
anaejibu kirahisi hivi sio mfanyabiashara wala hajui abc zake usipoteze mda
 
Mkuu, unaelewa maana ya "guvu ya soko?", Unaelewa maana ya biashara huria?. Sasa hapo tatizo ni wakenya wenye kuuza bei kubwa au tatizo ni wachina wenye kuuza bei ndogo?.

Mkuu, biashara ni ushindani, Kama wachina wanalipa Kodi na bado wanapata faida, tatizo liko wapi?, Kwanza wanawasaidia wananchi kwa kupata bidhaa za bei nafuu, kwanini hao wakenya wasiende kununua huko wanakochukua wachina Ili nao wauze bei za chini?.

Katika biashara, ni vitu viwili vitakufanya ufanikiwe, 1)Kuuza kwa bei ndogo, 2)Kuuza bidhaa zenye ubora.

Hao wakenya ni wabinafsi Sana, maua Yao huko Ulaya yanapendwa Sana kutokana na bei yake kuwa chini kuzidi maua yanayolimwa Uholanzi, kwanini Waholanzi wasiandamane kuzuia maua ya Kenya yasiingizwe Uholanzi?
 
Muwe mnaelewa kwanza habari kabla hujachangia kitu!!yaani mimi naenda china nanunua bidhaa kwa sh.100 bei ya jumla kiwandani, nakuja kenya naiuza kwa sh.1500!!huyo mchina analeta bidhaa hiyo hiyo na kuiza kwa sh.700!! Tena kwa reja reja!!hapo nitabuni mbinu gani ya biashara niweze kumshinda huyu mtu!!!
Kama anakushinda kupata bidhaa kwa bei ndogo, maana yake yeye yupo na "Competitive advantage" katika hiyo bidhaa, tatufa mbinu au biashara ingine ambayo wewe uko na " competitive advantage", hiyo ndio maana ya biashara. Usitake kulazimisha kufanya kitu ambacho wapo ambao wanakuzidi.
 
Mbinu ni kugundua inakuwaje yeye anauza bidhaa kwa bei ya chini wakati wote mnachukua kwa bei ile ile huko china na kodi,tozo za njian mnalipa sawa

Hicho kiwanda kinachokuuzia wewe bidhaa,ni cha kwake anachukua anakuja kuuza nchini mwako tena kwa reja reja!!hapo utamuweza wapi unafikiria ni kwanini Tz hao wachina wanaotaka kufungua magulio hapo kurasini wameanza kupigiwa kelele?!ndicho kinachoenda kutokea kariakoo watu wataliaaa!!!wao wachukue bidhaa kutoka kwenye viwanda vyao huko china,waje kuziuza hapa tena reja reja wewe unayekwenda kuvichukua china utawezana nao kwa bei?!!ki ufupi wachina mkicheka nao sana ni wapuuzi(wadhurumaji) muwekezaji anaiba maji/umeme kwa njia ya kihuni?!!
 
Kama anakushinda kupata bidhaa kwa bei ndogo, maana yake yeye yupo na "Competitive advantage" katika hiyo bidhaa, tatufa mbinu au biashara ingine ambayo wewe uko na " competitive advantage", hiyo ndio maana ya biashara. Usitake kulazimisha kufanya kitu ambacho wapo ambao wanakuzidi.
Yeye ndio mtengenezaji wa bidhaa hiyo,atuuzie huko kwao huyo huyo aje tena kuingilia soko letu kwa kuuza bidhaa hiyo tena kwa rejareja!!!fair competition iko wapi hapo?!!
 
Hawa makima sio wa kuwachekea safi sana Kenya piga mbwa hao.kwao ukifika hakuna namna yoyote utaweza kufanya kazi au biashara jinsi walivyojazana.Huku kariakoo wapo Hadi mawinga wa kichina hasta upanda wa vifaa vya umeme
 
Yeye ndio mtengenezaji wa bidhaa hiyo,atuuzie huko kwao huyo huyo aje tena kuingilia soko letu kwa kuuza bidhaa hiyo tena kwa rejareja!!!fair competition iko wapi hapo?!!
Mkuu, hiyo ndio biashara ya Dunia, Kama analipa Kodi na anawauzia wananchi kwa bei nafuu, hakuna tatizo lolote.

Kuhusu kiwanda ni chake, huo sio ukweli mkuu unadanganya, hakuna kiwanda kimoja chenye kutengeneza zaida ya bidhaa 3000 zinazoingizwa hapo Kenya toka China.

Bidhaa aina mbalimbali zinauzwa hapo China square, hao wachina wenye maduka hapo China Square ni wafanyabiashara tu, nao pia hununua bidhaa huko China na kuziingiza Kenya.

Tatizo kubwa la wafanyabiashara wa Afrika ni kutaka kupata faida kubwa kwenye bidhaa Moja, hii ni kutokana na kuwa na gharama kubwa katika uendeshaji wa biashara zao, anataka biashara hiyohiyo alipie ada ya shule ya watoto zaidi ya watoto 5, ajenge nyumba kubwa, aendeshe gari zuri, aweze kumiliki vimada watatu, anywe bia 6 Kila siku, michango ya harusi, michango ya misiba na takataka zingine kibao.
 
Waoga sana hao afu wanajifanya aggressive[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]....
Sasa wangekutana na mtifuano wa wahindi,wapemba, wachagga na wakinga ka hapo kariakoo cjui wangefanya nn maana k.koo ya moto sio kitoto
Ujinga ni kuruhusu mchina kuuza mabakuli Kariakoo kama mwekezaji. Huo ni umachinga ambao haukubaliki. Wao wanakuja kama Wawekezaji wenye mitaji mikubwa na uwekezaji wao uonekane. Sio kuchukua fremu Kariakoo na kushindana na Mkinga kuuza pair za kitenge au viatu.
 
Back
Top Bottom