Wafanyabiashara wa Ngara Watembelea Bungeni, Wakutana na Jafo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Wafanyabiashara wa Ngara Watembelea Bungeni, Wakutana na Jafo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

ZIARA YA MAFUNZO BUNGENI YA WAFANYABIASHARA WA NGARA YAWA NEEMA KWA BIASHARA ZA KANDA YA ZIWA.

04/09/2024, BUNGENI DODOMA

Baadhi ya wafanyabiashara wapatao 60 kutoka Jimbo la Ngara wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujifunza uendeshaji wa shughuri za Bunge, kuongea na viongozi wa Serikali juu ya maswala ya kibiashara sambamba na kutembelea Mji wa Serikali .

Wafanyabiashara hao wamefanya kikao cha kazi na MH. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa viwanda na biashara Mh. Seleman Jafo .

Kufuatia kikao hicho, serikali imepanga kutembelea Wilaya ya Ngara kukutana na Wafanyabiashara kwa ajili ya mafunzo mbalimbali ya elimu ya biashara na kutatua changamoto za kibiashara zikiwemo zile za KIKODI, SERA n.k

Wafanyabiashara kutoka Ngara wanatarajia kuutembelea Mji wa Serikali, kituo cha kisasa cha SGR, Chuo Kikuu kikubwa Afrika Mashariki na Afrika ya KatiChuo Kikuu cha Dodoma, Hospital ya Benjamini Mkapa pamoja na Soko la kisasa la Machinga jijini Dodoma.

Ziara hii ya mafunzo inaashiria mwanzo mzuri wa kuelewa na kumaliza changamoto za kibiashara ukanda wa Ziwa.

Wageni hawa wamepokelewa na Wabunge wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mh Ndaisaba Ruhoro (Mbunge Mwenyeji), Mh. Mwijage Mwenyekiti wa Wabunge wa Kagera, Mh Oliver Semuguruka Katibu wa Wabunge wa Kagera pamoja na Wabunge wengine.

Wenu
Ernest RUHUGU
Katibu wa Mbunge
Jimbo la NGARA
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.51.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.51.jpeg
    120 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.51(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.51(1).jpeg
    238.7 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.52.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.52.jpeg
    116.1 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.52(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.52(1).jpeg
    153.7 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.53.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.53.jpeg
    134.6 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.53(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.53(1).jpeg
    113.6 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.54.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 15.40.54.jpeg
    141.2 KB · Views: 7
Back
Top Bottom