KERO Wafanyabiashara wa soko la Sabasaba, Dodoma: Tunalipa ushuru, lakini miundombinu ya soko ni mibovu — ushuru unaenda wapi?

KERO Wafanyabiashara wa soko la Sabasaba, Dodoma: Tunalipa ushuru, lakini miundombinu ya soko ni mibovu — ushuru unaenda wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722

Baadhi ya Wafanyabiashara katika Soko la Sabasaba jijini humo wamelalamikia hali ya miundombinu mibovu ya mitaro ya majitaka, ambayo inasababisha maji chafu kupita karibu na maeneo yao ya biashara.

Wafanyabiashara hao wanasema kuwa tatizo hilo linaathiri afya zao na kuharibu shughuli zao za kiuchumi, hivyo wakiomba Serikali kuingilia kati haraka ili kutatua changamoto hiyo.

Soko la Sabasaba lina zaidi ya wafanyabiashara 7,000, ambapo baadhi yao wameripoti kuwa mtiririko wa majitaka karibu na biashara zao umepunguza idadi ya wateja kutokana na mazingira machafu.

Wafanyabiashara hao pia wamelalamikia kuhusu matumizi ya fedha za ushuru wanazotoa kila siku, huku wakihoji ni kwa nini miundombinu ya soko haikidhi hali ya usafi na usalama.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, mfanyabiashara mmoja alisema kuwa changamoto hiyo huwa kubwa hasa wakati wa mvua, hali inayowalazimu kufunga biashara na kurudi nyumbani. “Tunapitia changamoto kubwa sana ya majitaka.

Mvua zinaponyesha tunashindwa kufanya biashara, tunafunga na kurudi nyumbani. Tukikosa kufanya biashara, familia zetu hazipati chakula na watoto wanashindwa kwenda shule,” alisema mfanyabiashara huyo.

Kwa upande wake, Katibu wa Soko la Sabasaba, Nyamsuka Wisaka, amethibitisha kuwepo kwa miundombinu mibovu ya mitaro ya majitaka katika baadhi ya maeneo ya soko hilo.

Alisema kuwa tatizo hilo lipo katika hatua za kushughulikiwa na kuwa tayari wamekaa mara kadhaa na viongozi wa Halmashauri kujadili ukarabati wa miundombinu hiyo. “Ilikubaliwa kuwa miundombinu ya mitaro itasimamiwa na Halmashauri wenyewe ili ifanyiwe ukarabati,” alisema Nyamsuka
 
Hilo Soko si waliambiwa wahamishwe ili wajengewe soko la kisasa lenye miundombinu mizuri walikataa?!!! Fedha za Ujenzi zipo lakini wanawatumia wanasiasa kuwakingia kifua ilihali halmashauri ya Jiji inataka kujenga soko kubwa kama la Machinga pale Magomeni. Sasa hivi wanalalamika nini wakati wanajua fika soko halifai kutokana na Miundombinu kuwa sio rafiki?!! Wakati mwingine inatakiwa kufanyike Maamuzi magumu bila kuangalia, kwanza hapo sabasaba lilikuwa ni eneo la maonyesho ya biashara, wamevamia na kuligeuza Soko kwa nguvu. Watavuna walichopanda
 
Eneo lote siyo mali ya serikali
 
Kama wanalipa, watoe siku tatu lisafishwe, wasiposafisha waingie ofisi ya mkuu wa soko wamtoe wampe kipigo wafunge ofisi na wakatae kulipa ushuru, vurugu zinalipa sometimes
 
Back
Top Bottom