Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wafanyabiashara katika Soko la Tandika wameandamana wakilalamikia kuondolewa katika maeneo yao ya biashara, wakieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwapa changamoto na kuathiri shughuli zao za kiuchumi.
Wafanyabiashara hao wamesema wananchi wamechoka na manyanyaso wanayodai kukutana nayo, huku wakieleza kuwa msako unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa lengo la kufanya usafi na kupanga upya maeneo ya biashara unawarudisha nyuma kiuchumi.
Soma Pia: Wafanyabiashara Tandika wagoma kufungua Maduka, wakipinga Meza za Machinga mbele ya maduka yao
Katika kipindi hicho, baadhi ya wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wamachinga, wameondolewa katika maeneo waliyokuwa wakifanyia biashara, hali ambayo imeibua malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotegemea shughuli hizo kwa ajili ya kujipatia kipato.