Wafanyabiashara wa soko la Tandika waandamana kwa kuondolewa kwenye maeneo yao

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Your browser is not able to display this video.

Wafanyabiashara katika Soko la Tandika wameandamana wakilalamikia kuondolewa katika maeneo yao ya biashara, wakieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwapa changamoto na kuathiri shughuli zao za kiuchumi.

Wafanyabiashara hao wamesema wananchi wamechoka na manyanyaso wanayodai kukutana nayo, huku wakieleza kuwa msako unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa lengo la kufanya usafi na kupanga upya maeneo ya biashara unawarudisha nyuma kiuchumi.

Soma Pia: Wafanyabiashara Tandika wagoma kufungua Maduka, wakipinga Meza za Machinga mbele ya maduka yao

Katika kipindi hicho, baadhi ya wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wamachinga, wameondolewa katika maeneo waliyokuwa wakifanyia biashara, hali ambayo imeibua malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotegemea shughuli hizo kwa ajili ya kujipatia kipato.
 
Mbona vurugu zimekuwa nyingi? Huku Polisi kavamia watu tunduru, huku maandamano na kule wananchi waua askari wa maliasili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…