MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimeandika kwa masikitiko makubwa sana baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya marafiki zangu manufacturers kutoka nchini India ambao hutengeneza na kuuza vifaa vya hospitali. Kuna wenzetu wameingia tamaa na kuishia kudhulumu watu waliowaamini na kuwapa mzigo bila kulipa chochote kwa makubaliano ya kulipa baadae.
Hii ni tabia mbaya sana na inawaharibia wafanyabiashara wadogo wanaoanza kutoaminiwa. Malalamiko ni makubwa na tayari ubalozi wa India hapa nchini una taarifa za hawa watanzania wenzetu wenye tabia za kipuuzi. Kwa leo ninayahifadhi majina yao ila ninawasihi waongee na hao manufacturers na kukubaliana jinsi ya kulipa madeni.
Pamoja na lawama wanazotupiwa ila wahindi ni watu poa sana kufanya nao biashara. Kukuinua ni fasta. Binafsi nina ushuhuda wao. Vilevile ninawashauri wafanyabiashara kuwa waache upuuzi wa kushangilia ushindi kabla ya mechi kwisha. Ukipata faida iongezee kwenye biashara (recapitalize) hadi biashara iimarike kiasi cha kutosha ndo uanze mambo ya kununua magari, plot na kujenga nyumba. Kwa mfano hawa wanaotuhumiwa kukimbia na hela za watu ni watu wenye majina town kwa kuendesha magari mazuri na kuishi poa kumbe kuna dhuluma wanafanya.