Ijumaa, Agosti 28, shughuli za biashara katika sehemu za Nairobi CBD, Kamukunji, Gikomba na Nyamakima ziliathirika baada ya wafanyabiashara kufunga maduka yao na kuandamana kupinga kiwango kipya cha tathmini ya forodha kilichowekwa na Kenya Revenue Authority (KRA).
Kiini cha maandamano hayo ni kuongezwa kwa kiwango cha marejeo kinachotumika kwa 40-foot container ya consolidated cargo kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni, ongezeko la Sh700,000 au takribani asilimia 28.
Wafanyabiashara wanasema hatua hiyo itaongeza gharama za kuagiza bidhaa, kupunguza faida zao na hatimaye kusukuma bei za bidhaa juu kwa mlaji.
Waandamanaji walikusanyika maeneo ya Kamukunji na National Archives kabla ya kuanza safari kuelekea Times Tower, makao makuu ya KRA, wakitaka majibu kuhusu mabadiliko hayo.
Hata hivyo, walipokuwa wakielekea huko kupitia maeneo ya Moi Avenue, Parliament Road na Kenyatta Avenue, polisi walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya, hatua iliyosababisha taharuki na kuvuruga shughuli za kawaida katikati ya jiji.
KRA imesema Sh3.2 milioni si kodi ya moja kwa moja kwa kila container, bali ni kiwango cha marejeo kinachotumika katika usimamizi wa hatari na clearance ya consolidated cargo. Mamlaka hiyo inasema hatua hiyo inalenga kupunguza undervaluation, under-declaration na upotevu wa mapato ya serikali.
Tofauti na maeneo mengine ya Nairobi, biashara nyingi Eastleigh ziliendelea kama kawaida baada ya viongozi wa wafanyabiashara huko kuhimiza mazungumzo badala ya shutdown.
Wafanyabiashara wanapofikia hatua ya kufunga maduka na kuandamana hadi Times Tower, je, serikali inapaswa kusitisha valuation mpya na kufanya consultation upya, au KRA inapaswa kuendelea nayo licha ya upinzani wa traders?