BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wananchi wa hapa tumekuwa tukipaza sauti kwa muda mrefu kuhusu hali hiyo kuanzia ngazi ya uongozi wa mtaa hadi wilaya lakini hakuna mafanikio yoyote.
Naomba wajasiriamali waondolewe barabarani kwa sababu iko siku isiyofahamika gari litaacha barabara na kusababisha mambo ambayo sipendi kuona yakitokea.
Nashauri Serikali itafute eneo zuri na salama ambalo litawawezesha wajasiriamali kuweka bidhaa zao, siwapingi wenzetu kufanya biashara ila tatizo ni kutokuzingatia usalama.