Wafanyabiashara wanaochukua nguo Nairobi

nalamba yote

Member
Joined
Nov 21, 2017
Posts
56
Reaction score
53
Wakuu habari za Leo,Mimi sio mgeni sana hapa Jf Ila acc yangu ya mwanzo nimeshindwa kuitumia Kwa ss,..
Naomba kujua uzoefu Wa wafanyabiashara Wa Mpya za dukani hasa wale Wa Arusha na maeneo ya jirani wanaokwenda Nairobi Kenya kufuata nguo kwenye maduka ya jumla ni wapi maduka hayo yanapopatikana?....
Nataka kuanza hii biashara na fremu nimeshapata Ila naona nikinulia Nairobi itakuwa nafuu zaidi,tatizo sipajui wanapouza hizo nguo kwa bei nzuri huko Kenya na kila mfanyabiashara niliyemuuliza anasema lete hela nikienda nikuletee mzigo.
Najua Jf ni shina LA habari na wapo wazoefu Wa hizi mambo,...nisaidieni tafadhali.
Mtaji wangu ni milioni 7,nataka ninunue mzigo Wa milioni tano ili hizo 2 zinisaidie kwenye kodi ya TRA pale namanga.km kodi itazidi kidogo hapo kwenye milioni 2 sio mbaya nitapata ya kuongeza ziwe 3.
 
Hongera kwa hatua nzuri Mkuu, Kaza buti naaamin wadau wa pande hizo watatoa maelekezo yenye tija.
 
Duh.. wanafata falsafa ya JMK!
"Ili ule lazima uliwe kwanza.." - J.K.
 
Ningekua najua ningekupa Lead tatizo la watz wengi tuna roho mbaya sana niliwahi kutana na mtu anasema hadharani kabisa kua hawezi kusaidia mtu afanikiwe kama yeye,hii ni roho ya kishetani kabisa nani kakwambia you will last forever ? After all wewe sio wa kwanza kufanikiwa
 
Wadau wanaofata nguo mpya za dukani Nairobi huwa wananunua sehemu inaitwa Isilii......ni maeneo ya hapohapo mjini kati Nairobi, kunafanana kdg na kariakoo ya Dar.
Wauzaji wengi kama sio wote ni wakenya wenye asili ya kisomali, wako poa sana kwa maana ya uaminifu.
 
Ni kweli mkuu,hadi nimeandika hapa nishawauliza wengi sana ambao nawafahamu wanafanyaga hizo biashara lkn wanapiga chenga mkuu.
 
Mkuu ubarikiwe sana,Kwa maana hiyo nikifika hapo isilii nitafanikiwa hitaji langu?....Mungu akupe umri mrefu.
 
Mkuu ubarikiwe sana,Kwa maana hiyo nikifika hapo isilii nitafanikiwa hitaji langu?....Mungu akupe umri mrefu.
Yap utafanikiwa mkuu, maduka yote yapo ndani ya malls.......ukiingia ndani ya shopping malls mbili au tatu nadhani utakuwa umemaliza mahitaji yake.
Changamoto kdg itakuwa usafiri wa mzigo, unasafirisha kupeleka wp?
 
Pole mkuu, mimi sio mwenyeji Nairobi but ukitaka Kampala kuna uzi unaozungumzia biashara ya nguo Kampala
 
Napeleka Arusha mkuu,VP itakuwa shida sana kusafirisha?
 
Pole mkuu, mimi sio mwenyeji Nairobi but ukitaka Kampala kuna uzi unaozungumzia biashara ya nguo Kampala
Asante mkuu,nimeanza na Nairobi Kwa kuwa ni karibu kidogo na Arusha ila nadhani nikifanikiwa Nairobi next time nitajaribu na Kampala maana nimesikia kuwa pia huko kuna unafuu flani hv,ni kweli mkuu au wanapasifia tu?...naomba title ya Uzi huo Wa Kampala km hutojali au unaweza kunidokeza japo mawili matatu km sehemu zinapopatikana Kwa urahisi.
 
Napeleka Arusha mkuu,VP itakuwa shida sana kusafirisha?
Kuna kampuni (malori) yanasafirisha mizigo toka nairo kuja hapo arusha.....jina sikumbuki jaribu kudadisi hapo arusha mjini hasa kwenye vi noah vya kwenda namanga watakuwa wanajua.
Kusafirisha mzigo kwa lorry itakuwa nafuu kdg kuliko kwa kutumia ma bus.
 
Thanks much mkuu,naifanyia kazi leo,
 
Yap utafanikiwa mkuu, maduka yote yapo ndani ya malls.......ukiingia ndani ya shopping malls mbili au tatu nadhani utakuwa umemaliza mahitaji yake.
Changamoto kdg itakuwa usafiri wa mzigo, unasafirisha kupeleka wp?
Shikamoo!

EASTLEIGH ni fremu za maduka kama Kariakoo....ukifika Nairobi CBD ulizia matatu za EASTLEIGH nauli haizid 30kshs ukifika zunguka ufanye shopping ukimaliZa rud River Rd. (CBD) tafuta ofisi ya SPIDER wakabidhi mzigo na kiasi cha pesa watakachokuambia kisha utakuja kupokea mzigo wako TZ kwenye ofis zao SPIDER
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…