Tetesi: Wafanyabiashara wapatao 117 ndani ya Jiji la Arusha wanajiandaa kuteketeza zao lao la ngozi litokanalo na ng'ombe

Tetesi: Wafanyabiashara wapatao 117 ndani ya Jiji la Arusha wanajiandaa kuteketeza zao lao la ngozi litokanalo na ng'ombe

Starehe Kitandani

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
676
Reaction score
342
Habari nilizonyetisha mahala nikiwa napata supu ya ng'ombe ni kwamba Wafanyabiashara hao wapatao 117 ndani ya Jiji la Arusha wanajiandaa kuteketeza zao lao la ngozi litokanalo na ng'ombe. Watafanya hivyo siku za karibu kwani takrban sasa miaka 6 matajiri wao wa kuchukua ngozi hizo kila kukicha walalamika hawana pesa ya kuwalipa na wakati wanazichukua.

Wafanyabiashara hao wa Jiji la Arusha wanasema pamoja na zao hilo kuambiwa halina bei elekezi ambapo walikuwa wanalipwa kwa kilo Tsh 1,000/= miaka ile na kuporomoka mpaka kilo mojaTsh 100/= na hata hivyo hawalipwi na matajiri hao.

Mnyatishaji wa habari hii aliniambia karibu wachinjaji wote wanadai pesa zao bila ya mafanikio na wameshapeleka malalamiko yao sehemu husika lakini hakuna mafanikio yeyote😢

Kama ilivyo kawaida ya kukutana kila mwezi wamefikia maamuzi hayo wakiwa na machungu kabisa ya kukosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa Jiji la Arusha ingali wamewafikishia malalamiko hayo!!
IMG-20190710-WA0048.jpg

Natamani sana ningeona serikali ikiingilia kati suala hili la Wafanyabiashara hao wa Jiji la Arusha.
TASNIA YA NYAMA HII NI SEHEMU NYETI SANA KWA JAMII HIVYO MIMI BINAFSI NATAMANI SANA NIONE USHIRIKIANO WENU KUWANUSURU WAFANYABIASHARA HAWA HAPA WALIPO KWAMA🏃🏻🏃🏻🏃🏻

Naamini ushirikiano watapewa kabla ya maamuzi wanayotazamia kufanya,na ningependa kujua ya kwamba ngozi imekosa soko kabisa mpaka inafikiwa muafaka huu wa kuteketeza? Ama kuna nini ndani yake? Basi serikali iwawezeshe basi hata ile chama cha WANJAMUCO SOCIERTY iwatengenezee hata kiwanda cha kuchakata ngozi yao na wafanye biashara angalau kuliko kwenda kuchoma,Sina lingine ni hilo tu!
IMG-20190710-WA0049.jpg
 
Unaowaona katika picha ni kati ya wafanyabiashara wa nyama Jijini Arusha ambao siku chache zijazo watateketeza ngozi hizo ambazo zimedaiwa kukosa soko.
IMG-20190711-WA0000.jpg
IMG-20190711-WA0000.jpg
 
Huo mzigo umpelekee muitaly au muingereza uone hio product,
sio haya mafamba ya laki mpk laki na nusu k.koo
WA-IMG-20190704-287144a4.jpg

hii ni synthetic leather haikut hata robo ya full grain leather,
HAKUNA KIATU CHA LEATHER ESPECIALY FULL GRAIN LEATHER kikiwa kimefanyiwa procesing zote utakipata kwa chini ya lak 4 na ukikitunza utadumu nacho angalau miaka 10
 
Huo mzigo umpelekee muitaly au muingereza uone hio product,
sio haya mafamba ya laki mpk laki na nusu k.kooView attachment 1150979
hii ni synthetic leather haikut hata robo ya full grain leather,
HAKUNA KIATU CHA LEATHER ESPECIALY FULL GRAIN LEATHER kikiwa kimefanyiwa procesing zote utakipata kwa chini ya lak 4 na ukikitunza utadumu nacho angalau miaka 10

Kikao cha wachinjaji ndani ya Jiji la Arusha kiliendelea kukutana leo hii ndani ya chinjio la Arusha Meat & Company na bila shaka wale matajiri wa ngozi wameafikiana vema malipo ya ngozi kwa wale wadau wote wanaomdai
Hajaonekana tajiri mmoja tu mwenye kampuni ya SALEX COMPANY a.k.a SALIM ALLY na mwakilishi wake amesema yupo safari ila anaafikiana na wachinjaji ya kwamba anawalipa pesa zao zote!
 
IMG_20190717_164645_9.jpg
HUYU NDIYO MMOJA WA MATAJIRI WA NGOZI MNUNUZI WA NGOZI HAPA JIJI ARUSHA ANAMILIKI KAMPUNI INAYOJULIKANA KWA JINA YA NGOZI CENTER
 
Back
Top Bottom