Starehe Kitandani
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 676
- 342
Habari nilizonyetisha mahala nikiwa napata supu ya ng'ombe ni kwamba Wafanyabiashara hao wapatao 117 ndani ya Jiji la Arusha wanajiandaa kuteketeza zao lao la ngozi litokanalo na ng'ombe. Watafanya hivyo siku za karibu kwani takrban sasa miaka 6 matajiri wao wa kuchukua ngozi hizo kila kukicha walalamika hawana pesa ya kuwalipa na wakati wanazichukua.
Wafanyabiashara hao wa Jiji la Arusha wanasema pamoja na zao hilo kuambiwa halina bei elekezi ambapo walikuwa wanalipwa kwa kilo Tsh 1,000/= miaka ile na kuporomoka mpaka kilo mojaTsh 100/= na hata hivyo hawalipwi na matajiri hao.
Mnyatishaji wa habari hii aliniambia karibu wachinjaji wote wanadai pesa zao bila ya mafanikio na wameshapeleka malalamiko yao sehemu husika lakini hakuna mafanikio yeyote😢
Kama ilivyo kawaida ya kukutana kila mwezi wamefikia maamuzi hayo wakiwa na machungu kabisa ya kukosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa Jiji la Arusha ingali wamewafikishia malalamiko hayo!!
Natamani sana ningeona serikali ikiingilia kati suala hili la Wafanyabiashara hao wa Jiji la Arusha.
TASNIA YA NYAMA HII NI SEHEMU NYETI SANA KWA JAMII HIVYO MIMI BINAFSI NATAMANI SANA NIONE USHIRIKIANO WENU KUWANUSURU WAFANYABIASHARA HAWA HAPA WALIPO KWAMA🏃🏻🏃🏻🏃🏻
Naamini ushirikiano watapewa kabla ya maamuzi wanayotazamia kufanya,na ningependa kujua ya kwamba ngozi imekosa soko kabisa mpaka inafikiwa muafaka huu wa kuteketeza? Ama kuna nini ndani yake? Basi serikali iwawezeshe basi hata ile chama cha WANJAMUCO SOCIERTY iwatengenezee hata kiwanda cha kuchakata ngozi yao na wafanye biashara angalau kuliko kwenda kuchoma,Sina lingine ni hilo tu!