Wafanyabiashara wengi ukiwaulizia bidhaa ambayo hana anakasirika

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Najua sio wote, ila hii kasumba ipo sana, Nimeshuhudia hili kwa wafanyabiashara wengi. Japo nikiri kuna wengine wapo fair sana.

Unamuulizi bidhaa kama ikatokea hana anakujibu vizuri sina, njoo siku flani, lakini muungwana zaidi anakuelekeza kabisa Duka jingine na anakuambia asante na karibu tena, BIG UP kwa hawa watu.

Ila wengine kwa kweli ni changamoto, anakupokea vizuri tuu, ila unamtajia shida/bidhaa yako akiisikia tu kama hana, hata kama hatakujibu vibaya, kwa mtu mzima unaona kabisa response yake na uso kwenye feedback vimebadilika, sio tena yule aliyekupokea kwa tabasamu.

Kuna siku nipo na Rafiki yangu, tukaenda duka flani hivi k.koo, alikua na picha ya nguo flani hivi, alietuma ile picha kwenye mtandao mzigo wake uliisha, ndio akaamua aulizie kwenye maduka mengine. Tunafika pale tukapokelewa vizuri tu, tukamwambia kuna nguo tunayo kwenye picha tukuoneshe utuangalizie kama utakua nayo tuchukue.

Alikua na shauku kuiona akaitikia kwa uchangamfu, tukampa simu, ile kuangalia akajua hana, alibadilika ghafla akamjibu
"huyo alieituma ndio atakua anauza" akaweka simu mezani akaendelea na yake.

Jana nayo (ndio hiki kikanifanya niandike uzi). Jamaa katuma anauza bidhaa mtandaoni.

Nikamfuata inbox nikachagua moja wapo kati ya anazouza nikamtumia. Kwanza ile nimemtumia tu, hata kabla sijampa maelezo akaanza kutuma mapicha kama yoteee kwa furaha, nikamwambia nahitaji hii ila rangi flani(tofauti na aliyoweka) Akajibu: "Mimi rangi hio siuzi" Hata hata kabla sijareply, nashangaa kashafuta picha zake zote na kaniblock.

Nikacheke tu, asichojua ile rangi niliulizia tu kama ingepatikana ila nilikua tayari kuchukua rangi nyingine aliyonayo na tena na bidhaa zaidi.

Hivi ni visa vichache tu, ila hawa wanaojiita wafanyabiashara wana hii tabia sana, japo kwenye electronics sijaiona sana, nimeiona sana kwenye Mavazi, viatu n.k

Sasa unajiuliza huyu baadala ya kutumia nafasi hii kujua nini kinapendwa amepungukiwa atumie kama fursa ya kuvuta wateja yeye anakasirika?

Hivi sehemu kama hiyo unatarajia huyo mteja atarudi tena?
Unatarajia atamshauri rafiki/ndugu yake aje hapo?
Unafikiri atakutangazia sifa nzuri ya huduma yako?
Unatarajia nini kwenye biashara yako badala ya hayo?

Halafu hii pia inaletwa na kasumba ya wafanyabiashara wa Kibongo kuona huyu mteja mmoja atanipunguzia nini wakati napata wateja wa kutosha, lakini kumbe ungejirekebisha ungepata zaidi ya hapo, na kutojua biashara ni jina na mzunguko, huyo mmoja angeweza kukuletea wateja zaidi, lakini pia ungemhudumia vizuri angerudi tena na tena, mfano mimi nina tabia ya kurudia duka kama una huduma nzuri na pia nitakutangazia jina, sababu una deserve.

Mbaya zaidi unakuta anayefanya hivyo kawekwa tuu pale, anamgaribia boss.

Mwisho wa siku unaona kweli kupenda biashara sio kuweza biashara, na wachache wana kariba ya kuwamudu wateja wa namna yote, japo inajulikana pia kuna wateja wanakera sana na ni wasumbufu.

Kuna watu nishakutana nao, kwa kweli unahudumiwa vizuri, ukitoka hapo hata kama kakuuzia kwa bei kubwa au hamkufanya biashara ila Unaondoka ukiwa umeridhika kwa kadri ulivyopokelewa na ulivyoagwa.

Kuna watu wananyota tuu ya Umaskini.
 
Mkuu wengine wanaamka na mastress za familia zao wavumilie. Kuna mama mmoja hapa jirani yupo vizuri kiukweli anakuelekeza kwa vitendo inapopatikana bidhaa kama hana. Kuna wengine wapo makini ukimuuliza bidhaa na yeye aanakushawishi ununue alicho nacho.
 
Uyo aliyefuta picha baada ya kutaja rangi mshamba tuu uyo.

Na ndio maana Kuna makabioa yanasifiwa kwa biashara
Bila shaka na wewe ni katika kabila ambalo tunawasifia kibiashara
 
Mkuu wengine wanaamka na mastress za familia zao wavumilie. Kuna mama mmoja hapa jirani yupo vizuri kiukweli anakuelekeza kwa vitendo inapopatikana bidhaa kama hana
Kuna wengine wapo makini ukimuuliza bidhaa na yeye aanakushawishi ununue alicho nacho

Ni kweli wapo ambao ni waungwana na wana roho za nzuri na za kibiashara, Ukiona mfanyabiashara yupo tayari kukuelekeza sehemu nyingine ambayo sio yake huyo wivu na roho ya ubinafsi imempitia kando, Hawa watu ni wachache sana.
 
Kuna video moja ya jamaa (motivation speaker) toka SA anazungumza na wajasiriamali namna bora ya kufanya biashara.na jinsi watu wanavyokosea ni kufeli biashara.

Anasema daima zungumzia kwanini unauza bidhaa zako bei juu(thamani),na si kwanini unatakiwa kupunguza bei kumridhisha mteja.kama apple.

Ukitajiwa bidhaa ambayo huna,usipanick bali mshawishi mteja ni kwanini anunue ambayo iko dukani badala yake.

Upuka sana tabia ya kulia lia unapoombwa kushusha bei,hii inashusha thamani ya bidhaa.bali wewe piga siasa mpak mteja aridhike.

Pia anakwambia mteja anayeomba kupunguziwa bei huyo sio mteja wako, hajui thamani ya unachouza, ni afadhali uandike unaza saa 40k, haipungui. Kuliko kuwea 45 maongezi yapo.

HAWA WENGINE WANAFOSI BIASHARA HIZO NI KAZI ZA WATU, DUKANI KUTANA NA Mchaga, Mpemba, Muha utafurahi.
 
Big up,
Biashara ya leo bila kumalizana na mteja vizuri tena hizi zinazochipukia, kuchomoza utasubiri sanaa..

Binafsi dhana ya eti tuanzie juu halafu tushushane sijawahi ikubali na siwezi itumia...
Nataja bei Moja reasonable na ndio mwisho...

Unapoanzia mbali, kumbuka kuna wateja hawaulizi mara mbili, akiona bei ipo juu anasepa,
Na akitoka hapo, kauli yake ni moja tuu, "pale bidhaa zake ni juu" kumbe wewe ulikua unapima upepo,

Halafu ndio unaanza eti
"na wewe unaongea, au bei inapungua,"

Mwingine anataja range ya bei mfano
"kuanzia Elf 25 - mpaka 20"
huu ndio uswahili sasa, asa hio 25 umetaja ya nini?

Kumbuka unaposhusha bidhaa bei yako mbele ya mteja umekubali kuoshusha thamani pia mbele yake, huu ni udhaifu.


Na pili hii inakufanya uwauzie wateje bidhaa moja bei tofauti, kitu ambacho mimi naona sio fair na wakijua haitakuletea picha nzuri

Taja thamani halisi, isiokuumiza wewe wala mteja.
Kama ulivyosema mwambie kwa nini unauza kwa bei hio...

Kuhusu Mtoa mada, hao watu kweli wapo,
Ishatokea nikiwa na mshkaji alipojibiwa vibaya alitaka awake, Sababu namjua ni short temper nikamvuta nikamwambia.

"Mpotezee anastress zake huyo, we humuoni" Akaniangaria kwa kufura nikatabasamu tukasepa....

Siku zote
Epuka udhaifu wa kujibishana na Mdhaifu..
Au kumjibu mwenye hasira kwa hasira, Muoneshe kutojali.
 
Tatizo la wabongo hata ukimtajia bei halisi atataka apunguziwe tu. Yani hata ikiwa ni kwa 500 tu ila aone umekubali kushusha bei bila hivyo haridhiki na anaweza akaenda duka linalofuata ili akukomoe tu.

Imagine kitu umenunua 15k kwa jumla unataka upate margin ya 5k tu so unapaswa kuuza 20k ila mbongo lazima umwambie unauza 25k ili akiomba umpunguzie muishie kwenye 20k au izidi walau kwa buku 2!

Ukimtajia bei halisi ya 20k atataka umpunguzie umuuzie kwa 18k na hapo ukigoma anaenda duka linalofuata. Hii ni kwa uzoefu wa maeneo kama K/Koo!

Hivyo ni saikolojia ya wateja wa kibongo japo sahivi soko la Online limesaidia na linalazimisha bei fixed maana mteja na muuzaji hawaonani. Na bidhaa unakuta ni unique.
 
Mwingine anakujibu hicho kitu kimeisha au kilikuwa jana. Mimi kama mteja 'Mla ni mla leo,mla kesho ala nini' Tena bora ya mla kesho huyo aliekula jana yanihusu nini mimi ninaetaka kula leo?
 


Naamini ni Vusi Thembekwayo
 
Reaction ya mtu ni namna wewe ulivyomuuliza na unavyozidi kuzungumza naye, Sasa ni kweli wewe ni mteja unaniuliza kitu kwa dharau,anekutumia bidhaa alizonazo zote lakini bado unamuuliza kitu ambacho hakipo hapo kwenye list ni haki akasirike.!
Wakati ni kitendo cha wewe kuchagua kitu ulichoonyeshwa.!
 

Hujui biashara wewe!
 
Mkuu mbona unazungumzia katika mazingira yanayojulikana? Nisingeleta mada hapa, maana utakua umesababisha mwenyewe

Wateja wazinguaji wapo wanajulikana,
Wafanyabiashara wazinguaji kama hawa nao wapo sababu nao wanatoka kwenye jamii hii yetu....
 
... ni haki akisirike...
Ili iweje sasa? Nadhani mleta Uzi alikuwa akilenga watu kama nyie.
 
Ni kweli wapo ambao ni waungwana na wana roho za nzuri na za kibiashara, Ukiona mfanyabiashara yupo tayari kukuelekeza sehemu nyingine ambayo sio yake huyo wivu na roho ya ubinafsi imempitia kando, Hawa watu ni wachache sana.

Yeah!
Hii strategy wanaweza sana Wachaga.
Ikiwa utakuta Mangi hana bidhaa unayohitaji pale dukani kwake atafanya moja kati ya haya:
1. Atakwambia bidhaa haipo pale dukani lakini usubiri kidogo dakika chache maana ipo ktk store yake na atapiga simu fasta kwa Mangi mwenzake na bidhaa ilaletwa haraka toka duka lingine (siyo store).
Fedha uliyonunulia bidhaa watapeana baadaye

2. Atakuelekeza duka ambalo utapata bidhaa hiyo na mara nyingi itakuwa ktk kumuungisha Mangi mwingine mwenye duka.
 
khaaa,
Mkuu au ni wewe?😝😝😝😝😝

Sio kwenye biashara tuu, hata maisha ya kawaida, kiungwana mtu akija vibaya, kama huwezi kumrudisha vizuri, mwache arudi na ubaya wake, usimlipie ubaya..
 


Ili kumuwin mteja ndugu yangu wewe utafeli mapema sana! Jishushe maana unajua unataka nn hata kama hatakuachia hela yake next tym lazima aje kwako maana ulimhost vizuri ..Kalaghabaho.
 
Huwa nina amini kila mtu anakusudi lake duniani hao wameforce mambo maana mtu mwenye kusudi la biashara ndani yake
Anafurahia kuhudumia watu haijailishi ana stress au hana stress

Kusudi ni kitu ambacho unakifanya kwa furaha

#Ni Sawa na mwalimu anasema Mimi nimwemwacha mke wangu kitandani nimekuja kufundisha #wanarukia fani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…