Wafanyabiashara wengi ukiwaulizia bidhaa ambayo hana anakasirika

Wafanyabiashara wengi ukiwaulizia bidhaa ambayo hana anakasirika

Ni utafiti gani umefanya mpaka ukaja na hii conclusion?
Anyway rudia Tena huo utafiti wako.
 
Sahihi kabisa, kuna siku nilikuwa ninataka kununua laptops 6 kwa haraka, muda ulikuwa umeenda saa 10 jioni, nikawatafuta laptop city, namba nilichukua mtandaoni, wakapokea simu ila nilivyokuwa ninataja specifications jamaa akaniambia tuma kwenye WhatsApp kwanza tunafunga sasa hivi, nikawatumia walikuja kunijibu kesho yake saa 8 mchana, hapo nimeshanunua sehemu nyingine.

Nilichogundua ni aina ya wafanyakazi ambao tunaajiri, mtu mwenye biashara yake asingeweza kufanya hivyo
Screenshot_20200614-082949_WhatsApp.jpg
 
Najua sio wote, ila hii kasumba ipo sana, Nimeshuhudia hili kwa wafanyabiashara wengi. Japo nikiri kuna wengine wapo fair sana.

Unamuulizi bidhaa kama ikatokea hana anakujibu vizuri sina, njoo siku flani, lakini muungwana zaidi anakuelekeza kabisa Duka jingine na anakuambia asante na karibu tena, BIG UP kwa hawa watu.

Ila wengine kwa kweli ni changamoto, anakupokea vizuri tuu, ila unamtajia shida/bidhaa yako akiisikia tu kama hana, hata kama hatakujibu vibaya, kwa mtu mzima unaona kabisa response yake na uso kwenye feedback vimebadilika, sio tena yule aliyekupokea kwa tabasamu.

Kuna siku nipo na Rafiki yangu, tukaenda duka flani hivi k.koo, alikua na picha ya nguo flani hivi, alietuma ile picha kwenye mtandao mzigo wake uliisha, ndio akaamua aulizie kwenye maduka mengine. Tunafika pale tukapokelewa vizuri tu, tukamwambia kuna nguo tunayo kwenye picha tukuoneshe utuangalizie kama utakua nayo tuchukue.

Alikua na shauku kuiona akaitikia kwa uchangamfu, tukampa simu, ile kuangalia akajua hana, alibadilika ghafla akamjibu
"huyo alieituma ndio atakua anauza" akaweka simu mezani akaendelea na yake.

Jana nayo (ndio hiki kikanifanya niandike uzi). Jamaa katuma anauza bidhaa mtandaoni.

Nikamfuata inbox nikachagua moja wapo kati ya anazouza nikamtumia. Kwanza ile nimemtumia tu, hata kabla sijampa maelezo akaanza kutuma mapicha kama yoteee kwa furaha, nikamwambia nahitaji hii ila rangi flani(tofauti na aliyoweka) Akajibu: "Mimi rangi hio siuzi" Hata hata kabla sijareply, nashangaa kashafuta picha zake zote na kaniblock.

Nikacheke tu, asichojua ile rangi niliulizia tu kama ingepatikana ila nilikua tayari kuchukua rangi nyingine aliyonayo na tena na bidhaa zaidi.

Hivi ni visa vichache tu, ila hawa wanaojiita wafanyabiashara wana hii tabia sana, japo kwenye electronics sijaiona sana, nimeiona sana kwenye Mavazi, viatu n.k

Sasa unajiuliza huyu baadala ya kutumia nafasi hii kujua nini kinapendwa amepungukiwa atumie kama fursa ya kuvuta wateja yeye anakasirika?

Hivi sehemu kama hiyo unatarajia huyo mteja atarudi tena?
Unatarajia atamshauri rafiki/ndugu yake aje hapo?
Unafikiri atakutangazia sifa nzuri ya huduma yako?
Unatarajia nini kwenye biashara yako badala ya hayo?

Halafu hii pia inaletwa na kasumba ya wafanyabiashara wa Kibongo kuona huyu mteja mmoja atanipunguzia nini wakati napata wateja wa kutosha, lakini kumbe ungejirekebisha ungepata zaidi ya hapo, na kutojua biashara ni jina na mzunguko, huyo mmoja angeweza kukuletea wateja zaidi, lakini pia ungemhudumia vizuri angerudi tena na tena, mfano mimi nina tabia ya kurudia duka kama una huduma nzuri na pia nitakutangazia jina, sababu una deserve.

Mbaya zaidi unakuta anayefanya hivyo kawekwa tuu pale, anamgaribia boss.

Mwisho wa siku unaona kweli kupenda biashara sio kuweza biashara, na wachache wana kariba ya kuwamudu wateja wa namna yote, japo inajulikana pia kuna wateja wanakera sana na ni wasumbufu.

Kuna watu nishakutana nao, kwa kweli unahudumiwa vizuri, ukitoka hapo hata kama kakuuzia kwa bei kubwa au hamkufanya biashara ila Unaondoka ukiwa umeridhika kwa kadri ulivyopokelewa na ulivyoagwa.

Kuna watu wananyota tuu ya Umaskini.
Kitu kinaitwa customer service hapa kwetu Ni ndoto...sanasana wakishajua wateja wao Ni wengi Basi jeuri inazidi wanajibu wanavyotaka.
 
Sahihi kabisa, kuna siku nilikuwa ninataka kununua laptops 6 kwa haraka, muda ulikuwa umeenda saa 10 jioni, nikawatafuta laptop city, namba nilichukua mtandaoni, wakapokea simu ila nilivyokuwa ninataja specifications jamaa akaniambia tuma kwenye WhatsApp kwanza tunafunga sasa hivi, nikawatumia walikuja kunijibu kesho yake saa 8 mchana, hapo nimeshanunua sehemu nyingine.

Nilichogundua ni aina ya wafanyakazi ambao tunaajiri, mtu mwenye biashara yake asingeweza kufanya hivyoView attachment 1477976

Dah ..inakuaje unamletea nyodo mteja? Hahhaa! ...
 
Back
Top Bottom