CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Huwa naamini sana katika biashara zinazohusiana na ujuzi flani flani kwani najua hata kama utakosa mtaji pesa ila ujuzi wako utakusaidia kwenda kupata pesa ya kuanzisha biashara yako mwenyewe.
Nimekua na marafiki kadhaa ambao ni washonaji na wengine hata si marafiki zangu ila wengi kati yao tunapopiga story anakwambia biashara ni ngumu saivi anaweza maliza mwezi hajashona nguo hata 1 yeye wanakuja wateja wa kupunguza kiuno,kubana suruali za vijana,nk nk ambapo bei ya kuwafanyia hizo kazi ni vipesa vya vocha tu.
na ukiangalia mtu ana familia,ana hitaji na yeye kujihudumia lkn pia anataka atimize ndoto zake siku 1,kwahyo unakuta anakwambia nataka kuacha hi kazi niingie kuajiriwa au kufanya biashara flani flani ili aweze jikwamua,nk.
Leo naongea na Mshonaji au Mtu anaetaka kuja kuwa mshonaji siku 1 (msiohusika piteni kimya kimya asee,sio kila uzi unawahusu)
Biashara ya ushonaji ni kweli imekua ngumu sana kutokana na maisha tuliyopo,tupo ktk maisha ambayo n magumu yani mtu mpk anatamani angeweza avae tu shuka aende zake kazini ila ndio hivyo hawezi,Pona yetu ni "mchina" bwana tuseme tuwezavyo mimi kila siku naiombea CHINA hata siwadanganyi ndugu zangu.
Kupitia china tumeletewa nguo mpk za 1000 unazipata pale town,unapata nguo unajistiri maisha mengine yanaendelea,ikikaribia sikukuuu ndio kbsa watu tunakimbilia k.koo tunanunua nguo zetu (wajanja mnaziita maronya) ila ndio nguo tunazozimudu tunazivaa tunapendeza maisha yanaenda.
Zamani ilikua ikikaribia sikukuuu foleni kwa Fundi Ayubu ni hapa na kuleee,kila mwenye kitambaaa kanunua kapeleka kwa fundi kushona,kila mwenye anataka kupendeza anamuwaza FUNDI ESTER anaenda anashona, zikikaribia shule kufunguliwa foleni kwa mafundi sio za kawaida mafundi wako bizeee ni wanashona mpaka soksiii.
Leo hali ikoje"?? nani anaweza bei za kitambaaa + bei za mashono? nani? Jibu ni wapo ila ni wachache sana..sasa mafundi wanafanyaje? mafundi wao wameganda pale pale kusubiria oda za kushona magauni na mishono mingine mingine,nk.
Kwa tafiti zangu zisizo rasmi,Nimegundua kundi pekee linaloenda kushona nguo kwa mafundi awamu tuliyonayo (maisha magumu) ni wale wa nguo za Siku Maalum TU kama Sherehe nikimaanisha Harusi/vipaimara/wasimamizi wa maharusi (official code) ndio hao tu waliobaki wanaenda kushona nguo kwa mafundi,tuliobaki wengine wote kimbilio letu ni k.koo.
Nini chakufanya FUNDI?
Leo nataka uhame kutoka kwenye ushonaji nguo lakini sina maana uache kushona nguo Leo nataka nikwambie ufanye nini kupitia fani yako hiyo dhahabu ya ushonaji.
Binadamu anapovaa huwa havai nguo tu na kutoka kwenda zake anapoenda anavaa vitu vingine vingi ukiondoa nguo,Acha tudiscuss kimoja kimoja vile vichache japo vipo vingi ila leo ntawapa mifano ya vichache tu
Kofia
kuna kofia kina mama wanavaa wanapotoka hasa wale ambao unakuta alisuka nywele zmeanza kufumuka kwahyo ili kusubiri ifike week end akafumue hapa kati kati zamani walikua wakifunga vilemba ila siku hizi watu hawafungi vilemba tena kuna kofia ambazo zinashonwa na mafundi zinauzwa ni nzuri sana sana sana unazivaa ukiwa unaenda zako kazini,unazivaa ukiwa umelala,unazivaa wakati wowote ule utakaopenda.
Hizi kofia unaenda zako mjini unaponunulia vitambaaa unanunua kitambaa chako kizuriiii kisha unakata na kutoa idadi ya kofia unazotaka ambapo unaweza uza hizi kofia 5000-10000 ni kofia nzuri sana ambazo mteja akiziona hawezi chomoa kama kweli na wewe umejua zishona vizuri,kwa wiki utakosa wateja wa hizi kofia kweli? si kweli n lazima utapata wateja
Wengine hamjaelewa naongelea kofia zipi hizi hapa chini ndio kofia ninazoziongelea
Hizi kofia zinauzika vizuri na zina wateja,ila pia kama umezitamani hizo kwenye Picha Karibu PM kwa mawasiliano na namna ya kuipata 1 @7,000 bei ya jumla reja reja 1@10,000.
Scurf/skaf
scurf/skaf ni kikorombwezo ambacho watu wengi sana hupendelea kukitupia shingoni anapotoka kwenda kazini,hii tunavaa wanaume na wanavaa kina mama/dada unaweza kwenda mjini kama kawaida ukanunua kitambaa ukakata vizuri ukatoa skaf zako za kutosha kila skaf ukauza 3000 - 10,000 bei utajipangia kulingana na mbwembwe ulizoweka kwenye kila skaf uliyoshona,Kuna mechi za watani wa jadi unaweza vizia mechi y simba na yanga unatengeneza skaf za simba na skaf za yanga Mapema 11 upo mlangoni pale taifa unauza skaf zako Hivi unafkiri utatoka mule uwanjani hujauza skaf hata 1?? muhimu hakikisha unatengeneza bidhaa quality na sio za kutilia huruma huruma Mtu akitoa pesa yake ajivunie kuvaa kitu ambacho hakipatkani popote pale.
Vest
Kuna wale wapenda fashion hasa wanaoishi mikoa ya Joto ukitengeneza Vest nzuri za kushona ndani ukaweka kitambaa cha cotton then nnje ukashonea kitambaa chako ulichonunua mjini kisha ukai display vest yako ukaiuza 10,000 - 20,000 unafkiri hutoweza kuuuza? naamini ukiwa mshonaji mbunifu wakati unashona unakua unajua hii namshonea mteja wakiume kwahyo unaitia naksh za kiume,kama n vest ya kike unaitia naksh na unatumia vtambaa vyenye urembo wa kike kike.Ukimaliza una idsplay si lazima ushone vest 20 shona kulingana na mtaji ulonao shona hata mbili za kiume mbili za kike,mdogo mdogo unaendelea kuchanganya bidhaaa.
TAI
hivi umeshawahi kushika tai tunazozifaa sisi wanaume zipoje? unafkiri kuna teknolojia ya ajabu kwenye tai,basi siku 1 shika tai iangalie inavyoshonwa kisha ingia mjini chukua vitambaa vizuri vyakung'aa vya kutoa quality neck tie,tengeneza Tai zako za kutosha zi pack kisha tangaza una tai halafu uone utauza hizo tai au hautouza,Tunapigwa sana tai nakumbuka last time nimenunua tai kwa 30,000 hii ni kwasababu niliipenda ile tai ilikua unique mnoooo. Tai ni nyingi ila watu wanataka kitu ambacho ni tofauti,kwann wewe fundi unajua kushona usitushonee tai kisha ukatuuzia 5000 - 10,000 unafkiri hutouza? utauza nakuhakikishia muhimu zingatia Ubora na ukumbuke wavaa tai sio watu wa kisport sport "zingatia hilo"
T.shirt
Kama wewe n mpenda fashion hupitwi na kila fashion nadhani unakumbuka kuna kipnd ziliingia tshirt za kawaida kbsa za kichina ila kuna mafundi wajanja wakawa wanaziongezea thamani zile tshirt,ananunua tshirt bei ya jumla 5000 kisha anaipitsha kitambaa kati kati cha kitenge (mnazikumbuka eeh) halafu tshirt hyohyo anaiuza 15,000 wakati ameshonea kakipisi tu kakitambaa mbele ya tshirt..Kwanini na wewe usifanye hivyo? si lazima tshirt kuna vitu vingi unaweza vinunua ukavishonea kitu ukaviongezea swagg ukauza ukapga pesa,Inawezekana Amua tu.
Carpet
Umeshona vitu kibao umekatakata mavitambaa mengiii yapo hapo yamerudikana kwanini usishone vile vikapet vya kuweka mlangoni vyakufutia miguuu,unganisha hvyo vipisi toa vikapet vyako kadhaaa uza kila kikapet 3000 utapata pesa bana wanunuaji wapo usifkiri kila mtu ana hela ya kununua hcho kikapet 5000 to 10000 wewe tengeneza vyako uza kwa 3000,utapiga pesa vizuri tu.
Mifano ipo mingi sana ya kushona au kununua hizo za madukani na kuzishonea vitu kwa juu na kisha unaziuza tena,hela zipo guys biashara au fani ya ushonaji ni nzuri sana na ina mianya mingi ya kupiga msijifunge ktk ushonaji wa nguo tu Tafuta mtaji wako fata vitambaa vyako tofauti tengeneza vitu vyako Kisha uza.
Raha ya hivi vitu ni kwamba unauza vitu ambavyo vinatumika na kila mtu,kofia wanavaa wamama,wadada,wabibi,skaf wanavaa wadada/wababa/wababu,tai nk nk kwahyo ukijiongeza ukafungua akaunti yako ya kulipia ya FACEBOOK na INSTAGRAM dear friend wateja watakuja na utawapata wengi
"Usiache kazi unayoifanya jaribu kuwaza nini ufanye ili usonge mbele zaidi,Unachokifanya sasa ni bora kuliko unachofikiria kukifanya"