Natimiza ahadi yangu Mtanzania halisi kwa kiapo cha kuipenda,kuitumikia ,kuitetea na kuilinda nchi yangu ya Tanzania.
Ni fahari ya kujivunia kuwepo kwa mfalme wa kiarabu katika chaguo lake katika ardhi ya Tanzania. Nchi za Afrika zenye vivutio vya utalii visivyopishana sana na vyetu hapakuwa na upenyo wa kutushinda. Ni dhahiri Tanzania imesheheni uzuri wa vivutio.
Ni tosha kuthibitisha kuwa Tanzania ipo juu,juu,juu zaidi.
Ni aibu kumkosa . Seuze tunae?!
Tunajivunia , Tunampenda ,Tunamuenzi .
Je? Ni mpita njia? La hasha! Tokea mwaka 1992 mpaka sasa amedumu kwa miaka 27.
Si mgeni tena ni mwenyeji. Tokea uhai wa Baba wa Taifa. Ni sisi.
Emirates airline inayomilikiwa na ndugu ya mfalme huyo ambayo ilishiriki kikamilifu kuutangaza mlima kilimanjaro. Miaka ya nyuma niliwahi kupanda ndege hiyo kutoka dubai kuja dar kwa mara ya kwanza niliuona mlima kilimanjaro kwa juu. Na walitoa maelezo yake huku tukiupita. Sasa imesitishwa.sifahamu kwanini na sijui kwa zile routes za kutoka Nairobi kama zinaendelea kuonyesha Mlima Kilimanjaro.Wengi wa watalii wanatoka huko makundi ya wafanyakazi wa makampuni kuja katika utalii wa hapa nchini na kuupanda mlima Kilimanjaro. Na mengine mengi ambayo Sisi tunaendelea kwa ulaini kula matunda ya ardhi yetu kwa kupitia chaguo lao.
Hawapo hapa sababu ya shida zao ,wala kuwapokea sio ujinga wetu. Tusiwe wapayukaji tukasahau thamani ya uwepo wao. Tuwe Makini na tusiende kombo kwa dhana za upotoshaji.
Enzi za Baba wa Taifa Watanzania tulisifika na kujijengea heshima kwa tabia za upendo na amani husan kwa wageni. Nakumbuka ilikuwa maagizo kuwa mgeni ahudumiwe asipate usumbufu kama mwenyeji.Foleni ya sukari akitokea mgeni huenda moja kwa moja akapata huduma.Watu walikuwa maridhia, sasa tunashuhudia hakuna kumpisha mzee katika kiti.Adabu na heshima zile zimepotea.
Namsifu Baba Magufuli amerudisha heshima ya watanzania. Tukienda Kenya wanatufurahia Tunaaminika ni watu wasio na vitisho, ghasia wala usumbufu.na kwengineko.
Ni matumaini yangu Mheshimiwa Rais Magufuli utaliona na katika Ujenzi wa Taifa letu basi utamaliza vikwazo,Fitina na Usumbufu uso na lazima na Wageni wetu wakae kwa Furaha na Amani.
TUMTANGULIZE MUNGU KATIKA KILA JAMBO LETU
MUNGU IBARIKI ARUSHA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA