MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mchina juzi alifukuzwa Kenya kwa kosa la kuwatukana Wakenya, huku JF hakukukalika kwa jinsi Watanzania walichekea tukio hilo. Lakini cha kushangaza wao kama ilivyo kawaida huwa hawajiangalii, tusi la kibaguzi dhidi ya Mkenya mweusi linawahusu pia, yaani kuwa na akili ndogo ni laana.
Sasa taarifa zimejitokeza jinsi Wachina huwapokeza Watanzania kichapo cha mbwa , sasa ipi ovyo, kutukanwa au kupokea kichapo cha aina ya kung-fu na bado unanyimwa mshahara na kufutwa kazi.
Hii imebidi hadi waziri wao ameingilia kati na kuwafukuza baadhi ya hao Wachina.
Cha msingi Waafrika tujitambue, tunaweza kuwa na tofauti zetu za ndani, lakini pale Mwafrika mwenzetu anabaguliwa, inabidi tulaani wote kwa pamoja. Juzi nilichukia sana kuona Mghana ameuawa kule China kisa kapata mchumba wa Kichina.
Inafaa Mchina akija na kung-fu zake hizo, nyanyua jiwe mpige nalo, tafuta mawe kote umnyeshee, aki ya nani sipigwi mimi hata kama wewe ni Jet-Li
----------------------
Uamuzi wa kuwafukuza Wachina hao ulitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye mradi huo, unaotekelezwa na Kampuni ya China Railway 15 Beaural Group Corporation Ltd.
Wakati akiendelea kukagua mradi huo, Waziri Kamwelwe alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Matundasi, ambao walimweleza manyanyaso wanayoyapata, ikiwamo kupigwa, na wasimamizi wa mradi huo, raia wa China.
Mmoja wa wananchi hao ambaye ni wafanyakazi kwenye kampuni hiyo, Wilson Pawa, alisema makandarasi hao wanawanyanyasa kwa kuwasingizia kuwa wanawaingizia hasara na ikitokea wakabishana huanza kuwapiga kung-fu na kutishia kuwaua kwa risasi.
"Hawa Wachina ukimaliza kazi wanasema umewatia hasara. ukibisha wanaanza kutupiga kung-fuu na wanatutishia kutuua na wanatupiga kweli kweli si mchezo. Mimi hadi sasa nina uvimbe na maumivu makali na nimechukua PF 3 (fomu ya matibabu kutoka polisi) kwa ajili ya matibabu," alisema Pawa.
Naye Mapuli Mbumba, ambaye ameajiriwa na kampuni hiyo katika nafasi ya dereva, alisema Wachina hao wanaajiri bila kuwapatia mikataba ya ajira na kila ikifika mwisho wa mwezi, wanakata mishahara yao bila sababu za msingi kinyume cha makubaliano.
Alisema kutokana na unyanyasaji huo, wananchi hawana uhusiano mzuri na kampuni hiyo, jambo ambalo linahatarisha amani miongoni mwao.
"Tunajua sheria inataka wakituajiri watupatie mikataba ya ajira, lakini wenzetu hawa hawatoi mikataba na mwisho wa mwezi wanatukata mishahara na wakiamua wanakufukuza wanavyotaka. Kwa kweli wanatunyanyasa sana," alisema Mbuba.
Diwani wa Matundasi, Kimo Choga, alisema mbali na kero hizo, pia kuna tatizo upande wa magari yanayotumiwa na Wachina hao kujenga barabara kuwa ni mabovu na yanaweza kuhatarisha usalama wa wananchi.
Alisema magari hayo hayana taa, vioo vya kutazamia nyuma (site mirror) na taa za ishara (indicator), hali ambayo kama yakiongozana na gari lingine dereva hawezi kujua kama limesimama, hivyo ni rahisi kusababisha ajali.
Choga pia alidai kuwa makandarasi hao hawajali hata kumwaga maji kwenye barabara zinazojengwa na zile zinazotumika wakati wa ujenzi hali ambayo inasababisha makazi ya watu kujaa vumbi na kuhatarisha afya za wananchi.
Raia wa China watimuliwa kwa kuwapiga makonde Watanzania