Wafanyakazi nane wa BoT kortini Dar kwa kughusi vyeti

Ni mwanzo mzuri. Lakini ni hekima kucheki 1st degrees, masters na PHD pia kwani huko ndiko kwenye makanyanga ama mafefe ya kutisha. Vijana wengi wenye vyeti feki wako BOT, kampuni ya sigara na serkalini haswa bungeni aka (Dr Nchimbi and his group)

Tanzania kupata maendeleo ni ndoto kwani VIHIYO ni wengi kuliko wasomi wa kweli.
 
Mamuzi ya mahakama yatakuw ahivi ifuatavyo hawakufanya kwa nia mbaya kwahiyo wachiwe huru na kulipa faini na kwa wale watakaoamini kutakuwa na hukumu ya kutowa funzo kwa wengine tulisahau hilo naweka usha hidi huu tusubiri the out come.
 


Hivi huyu "Dr." Nchimbi alifanyia wapi hiyo "PhD" yake? Kuna mwenye biography yake hapa JF?
 
Wazo Mbadala: Ndugu wadau, la kufanya ni kuanzisha libeneke jipya hapa. Mwenye Data za watoto wa vigogo aka vipapa walete hapa jamvini kisha tuzipigie kelele kwa kwenda mbele. Kama ni just mere speculation, then we have to keep quite. Leteni data zao kama matokeo, shule walizosoma na grade zao za kweli.
Kuhusu PhD za kikanjanja, namwomba mwkjj atoe makal hiyo kwenye kijarida chetu cha kila wiki. Naomba kuwakilisha.
 
Sidhani kama Benno Ndulu anastahili sifa yoyote genuine katika hili la walioghushi vyeti.

Yes he makes some difference. But as statisticians say or ask. Is it significant? Siamini. Kule BOT kuna makubwa ya kushughulikia, tena ya haraka.

Hili si kubwa, wala si la haraka. Ni ujuha mtupu, kama wa Taifa stars kushinda bao 4 huko Mauritius. Ushindi ambao hauleti significant difference katika michuano hiyo.
 
Hivi huyu "Dr." Nchimbi alifanyia wapi hiyo "PhD" yake? Kuna mwenye biography yake hapa JF?

Commonwealth Open University. CV ya Nchimbi unaweza kuipata kule kwenye website ya bunge.
 
Issue kama hizi humalizwa na mapinduzi na si vinginevyo...Sana sana ni kujenga mazingira ya uchafukaji wa amani
 
Kama watu wanaweza kupata kazi kwa kutumia vyeti feki kwenye taasisi nyeti ya nchi kama BOT then......LORD HELP US! Na sioni ni kwanini hao walihusika kutoa hizo ajira wasiburuzwe kortini nao.
Pia nashindwa kuelewa kughushi cheti kunaingiliana vipi na rushwa hadi TAKUKURU ndio wawe mstari wa mbele kwenye suala hili, surely there is a difference btn forgery and corruption.
 
........ Nasema Tanzania hatuna press! Inawezekana 50% ya mambo tunayoyapigia kelele hapa yanatokana na misinformation. I tell you. Ohooo! Hakuna viable press! Hakuna anaejua kinachoendelea Bongo kwa kusikiliza hii media uchwara....

.........hapo tuko pamoja mkuu........good observation!
 
Inabidi mahakama iwaruhusu warudie mtihani uku wanaendelea na kazi...
Ingawa nao naona walikuwa wamebweteka sana...toka 2001 and 2002 hawaja rudia mtihani walikuwa wanasubiri nini...unapata kazi harafu unaanza fanya masomo ya jioni...

Kisha unafanya mtihani na kucover credit zako kisha unakuwa sawa.....kabisa...hata kama wakisema wewe unatoka na cheti chako halali...
 

....inaelekea wee Buswelu mtaalam wa hayo mambo eehh.....kwi kwi kwi kwi
 
Mbona wote ni wanawake? au ndiyo rushwa ya RAV4? tehetehe
 
....inaelekea wee Buswelu mtaalam wa hayo mambo eehh.....kwi kwi kwi kwi

Nop just thinkig the other way around...sasa muda wote walikuwa wanafanya nini....unajua ni ujinga sana....wakihukumiwa kwa mie ntabaki na furaha na wakipewa muongozo kama wangu ambao haiwezekani...nayo ni pouwa...

Jaribu kufikiri umefeli form 4...huna mood ya kurudia muda huo baba(Mungai) anakwambia i can do this for u...anafanya sasa wewe unabidi ujiongeze baadae....tena the same yr ange jisajiri...akaanza kufanya...2002 angekuwa na cheti chake..haya yote yasinge mfika...tena walikuwa na God Father wao RIP balali....leo hii wasingekuwepo kwenye kundi hili.
 
Hizi habari za ufisadi, wizi na kugushi.... Zinanikumbusha kisa kimoja kilitokea zamani kidogo...! Kisa chenyewe kinasema hivi:

kijana mmoja kafikishwa mahakani kwa kosa la kumuibia dada mmoja mkufu wa dhahabu, na kuumeza tumboni, baada ya kusomewa kosa lake na kumuonyesha uthibitisho wa picha za x-ray alizofanyiwa hospitalini ili kumthibitishia kosa lake.

Hakimu akamuuliza mshitakiwa, Kama ana lolote la kujitetea?

Kijana: Ndio bwana Hakimu ninalo neno moja nataka kusema...!

Hakimu: sawa kijana unaweza kujitetea...!

Kijana: (Akaanza). Bwana Hakimu ningependa kuishukuru serikali yetu tukufu kwa kuweza kuweka vifaa vizuri vya kufichuwa vitu vikiibiwa na wezi kama mimi na hata vikifichwa tumboni kwa kumezwa, lakini ninauliza jambo moja tu Bwana Hakimu.

Kwanini serikali haijaweka vifaa vya X-RAY vya kufichuwa WAHESHIMIWA WANAO IBA MAMILIONI YA FEDHA AMBAZO NI MALI YA UMMA WA WATANZANIA WOTEE?!! PAMOJA NA WALE WENYE KUGUSHI NA KUFOJI DEGREE ZA PHD NA VYETI VYENGINE AU HUO NAO SIO WIZI NA UFISADI!?

Asanteni Bwana Hakimu, sina zaidi...!
 
hivi hawezi kupewa muda ili waje na vyeti halali?
nauliza tu
 
Kama kawaida ya bongo, tunahangaika na "vidagaa" vilivyofoji vyeti vya "fomu foo" tunawaacha "kambale" na "sangara" waliofoji madigirii hadi mapiechidii! Halafu watoto wa vigogo wako wapi kwenye hiyo orodha? Huyo binti wa mzee Mungai ndiyo "watoto wa vigogo" ambao magazeti yanajinadi wamebambwa huko BoT kwa kughushi vyeti? Bado kazi ipo, kubwa sana!
 
hivi hawezi kupewa muda ili waje na vyeti halali?
nauliza tu

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha jamani JF kuna mambo...wapewe nafasi waje na vyeti halali.....ndio hapo mtakapo pumzika.
 
Sasa!! Kama Form Four wamefoji vyeti na kazi yao ilikuwa kuhesabu Pesa hawawezi kufoji hata mahesabu ya pesa zenyewe? Maana BOT kuna mabilioni na hawa wasio na vyeti si ndio watachanganya mambo! Hii nchi kweli ya mazingaombwe.

Tunamuamini sana Prof Ndulu lakini hoja tuliyokuwa tunaitamani sana aiseme ni kuhusu watoto wa Vigogo walee 16 walioajiliwa kiutatanishi sio hawa. Mwambieni ayalete yale majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…