Feld Marshal Tantawi
JF-Expert Member
- Dec 24, 2014
- 655
- 1,069
Benki ya CRDB imezindua kampeni maalumu ijulikanayo kama “Jiachie Utakavyo” ambapo wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi sasa kufurahia riba ya hadi asilimia 14. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati, Boma Raballa alisema benki imefanya maboresho makubwa katika mikopo ya wafanyakazi ili kuwapa unafuu na kuwawezesha kufikia malengo yao waliyojiwekea.
“Jiachie Utakavyo inamaanisha kuwa wafanyakazi sasa wana wigo mpana zaidi wa kukopa, kwa gharama nafuu, kwa muda mrefu na uhuru wa kuchagua wanachotaka,” alisema Boma Raballa. Raballa alisema pamoja na kumpa uhuru mteja wa kujiachia kwa kuutumia mkopo atakavyo, Benki ya CRDB pia imempa uhuru mteja kuchagua muda wa kulipa mkopo anaoendana na matakwa yake na kiwango cha riba anachotaka kulipa.
“Kwenye jiachie utakavyo mteja ana uhuru wa kuchagua muda wa kulipa iwe ni mwaka 1, 2, 3, mpaka 7, na vivile mteja atakuwa anachagua riba anayotaka kuanzia asilimia 14 mpaka 16,” alisema Boma Raballa huku akibainisha kuwa kampeni hiyo ya “Jiachie Utakavyo” inawapa fursa wafanyakazi kukopa hadi shilingi milioni 100.
Akizungumzia kuhusiana na maboresho hayo ya mikopo ya wafanyakazi, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili alisema Benki ya CRDB inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi wa taasisi za Umma mna sekta binafsi, hivyo basi maboresho hayo ni motisha kwa wafanyakazi kusaidia kufikia malengo yao.
“Tunafahamu changamoto tulizopitia katika kipindi hiki, na wafanyakazi wetu wamekuwa mstari wa mbele kukatika kutuhudumia katika kila nyanja, kampeni hii ya Jiachie Utakavyo ni sehemu ya shukrani kwa wafanyakazi wote, lakini pia kuwasaidia kufikia malengo yao,” alisema Adili.
Kwa upande wake Meneja mwandamizi Mikopo ya Wafanyakazi, Farida Hamza alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyakazi wote nchini kuchangamkia fursa hiyo ya “Jiachie Utakavyo”, huku akibainisha kuwa mteja ana uhuru wa kutumia mikopo hiyo atakavyo ikiwa ni pamoja na kulipia ada za Watoto, kijiendeleza kimasomo, kuanzisha na kuendeleza biashara na matumizi mengine apendayo.
“Mikopo hii si kwa wateja wa Benki ya CRDB tu ni kwa wafanyakazi wote nchini, kama mfanyakazi anamkopo benki nyengine, Benki ya CRDB inautaratibu wa kununua mikopo ili kuwafanya wafanyakazi wote waweze kujiachia watakavyo na Benki yao pendwa ya CRDB,” alisema Farida huku akibainisha mikopo hiyo inatolewa ndani ya saa 24 mteja napokamilisha maombi ya mkopo.
Ili kupata mkopo huo wafanyakazi wanatakiwa kutembelea tawi la Benki ya CRDB lililo karibu na kujaza fomu ya maombi ya mkopo ambapo atatakiwa kuambatanisha vielelezo vifuatavyo; Kitambulisho kinachotambuliwa - cha utaifa/ kura/ leseni ya udereva na kitambulisho cha kazi, Hati ya mshahara (Salary slip) iliyothibitishwa kwa kipindi cha miezi mitatu, Mkataba wa kazi/ barua ya uteuzi, barua ya utambulisho, barua ya uthibitisho kazini.