Mmi pia nitampa kura yangu Jakaya mwana wa Kikwete .Anaelezeka.kama wafanyakazi wameamua hivyo.....nami sinabudi kuwaunga mkono
Mgaya sasa amekuwa muelewa.aendelee hivyohivyoJana mgaya alitoa tamko na kukana habari iliyoandikwa na TAnzania daima kuwa "TUCTa yamjibu Kikwete"
Kataika gazeti la leo Nipashe Mgaya amesema Jk amesikiliza kilio cha japo hajafikia lengo lao
Mgaya amesema hapo kawajali wafanyakazi kura watampa
BABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one
Rais Jakaya Kikwete
Na Waandishi Wetu
Wakati Shirikisho la Vyama vya Wanyakazi nchini (TUCTA) likidaiwa linajipanga kutoa tamko la kuwataka wafanyakazi wote nchini kutompigia kura Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, inaonekana mambo ni kinyume.
Sehemu kubwa ya wafanyakazi wanaeleza kufurahishwa na utawala wa JK, hivyo kuwa tayari kumuongezea kipindi kingine cha uongozi cha miaka mitano (2010-2015).
Wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili kwa wiki nzima iliyopita, Dar es Salaam, walieleza kufurahishwa na kazi ya JK aliyoifanya Ikulu kwa miaka mitano, hivyo wanaamini ataendeleza mazuri endapo ataongezewa kipindi kingine.
Walisema kuwa Rais Kikwete ameweza kuonesha moyo mzuri kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mara kwa mara pia kukabiliana na ufisadi, hivyo hawaoni sababu ya kuliunga mkono TUCTA endapo litasema JK asipigiwe kura.
Baadhi ya maoni ya wafanyakazi kama walivyozungumza ni kama ifuatavyo;
ITUS BILLA
Mfanyakazi wa Kampuni ya Big Bell.
Anasema: "Nafurahia kipindi chote cha Kikwete kuwepo madarakani, maana mengi aliyoahidi ametekeleza. Nawashauri Watanzania wenzangu tumuongezee kipindi kingine aweze kuleta maendeleo zaidi. Kuhusu nyongeza ya mshahara mimi naona maisha yatakuwa yale yale kwani kila mshahara ukitangazwa kupanda na bidhaa nazo zinapandishwa."
Itus Billa
SULEIMAN MAZINGE
Anasema: "Utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni mzuri kwani nchi ina amani na hakuna njaa wala migogoro na hilo ndilo jambo kubwa, mambo mengine ni majaaliwa. Kuhusu ongezeko la mishahara hapo hakutakuwa na jipya kwani uzoefu unaonesha mishahara ikipanda na huduma nazo zinapanda."
Suleman Mazinge
ANNA LUWENA
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri na anaomba uendelee ingawa hauna tofauti kubwa na tawala zingine zilizopita. Kuhusu kupanda kwa mishahara ni bora ingebaki palepale kwani ongezeko la mishahara litasababisha kuongezeka maradufu kwa gharama za huduma mbalimbali."
Anna Luwena
HUSSEIN MAKUBI
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri kwani ameendeleza mazuri yaliyoachwa na marais waliopita. Kuhusu mishahara mwanzoni wananchi watafurahia ongezeko hilo lakini siku zinavyokwenda huduma nazo taratibu zitapanda na kufanya hali kuwa ile ile."
BABY OMARY
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri hakuna dosari kubwa iliyojionesha ukilinganisha na tawala zilizopita.
Ongezeko la mishahara linatokana na kusonga kwa dunia lakini halina uhusiano wowote na ubora wa maisha kwani hapo zamani mfanyakazi alilipwa 6000/ (elfu sita) mfanyakazi huyo sasa hivi analipwa 600,000/ (laki sita) lakini maisha yake ni yaleyale afadhali ya zamani.
Baby Omary
HADIJA HASSAN
Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom anasema: "Utawala wa Rais JK ni mzuri na hasa kwa kuwa ametoa ajira kama alivyoahidi, hivyo kuwakomboa Watanzania. Ongezeko la mishahara anasema litakuwa na mafanikio kwa wenye malengo lakini wasio na malengo wataendelea kuumia."
GHONCHE MATEREGO
Katibu Mtendaji wa BASATA, anasema: "Rais Kikwete uongozi wake ni mzuri sana pia ni mtu anayeona mbele zaidi ndiyo maana anawapa vijana kipaumbele tena anapenda kuwarithisha ili baadaye wawe viongozi wanaofaa kuongoza nchi. Amekuwa ni mchango mkubwa sana kwa vijana, lakini hajawaacha wazee anawataka kuelimisha vijana wao ili waweze kujikwamua kimaisha.
"Kwa upande wa mshahara kuongezwa hilo nalo ni jambo la heri na serikali imetimiza ahadi yake kwani kilikuwa ni kilio cha siku nyingi na sasa imefikia mahali na kuongeza tunashukuru kwa kutimiza ahadi hiyo."
MBAZI OMBENI
Karani wa BASATA, anasema: "Utawala wa Rais Kikwete siyo mbaya sana lakini kuna ahadi ambazo naomba kama akichaguliwa tena awamu ya pili azitekeleze. Shule za Kata zimejengwa nyingi lakini vitendea bado tatizo, naomba aliangalie hilo pamoja na mfumuko wa bidhaa sokoni.
"Suala la mishahara kuongezwa nashuru kwa sababu kilikuwa kilio chetu cha siku nyingi."
zao ni kwa
SOURCE: Global Publishers aka. Shigongo
BABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one
Sishangai watakaompa kura kikwete maana wengi ni wale waliokosa elimu hivyo wakazibwa milango yao yote ya FAHAMUBABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one
Watu wanajitolea tu,pole wewe unaelipwa kazi unayo siku usipofanyakazi mwajili atakunyima malipo.sijui kama anakulipa KCC cha TUKTA au la.Bill, unamtumikia nani na umelipwa bei gani?
How come majibu yote yafanane hivyo, i smell a rotten kitten here!.
HaaahaTetee,halooo.REV kwa kutukana bwana.ndizo zako tumekuzoea.PowaaaBange hizi!
Nia tunayo,elimu tunayo,sababu tunayo.kazi ikiyobaki ni moja tu.TUTAMPA KURA ZETUSishangai watakaompa kura kikwete maana wengi ni wale waliokosa elimu hivyo wakazibwa milango yao yote ya FAHAMU
Angalia usivunje mkono.Ya nini kupata kiharusi ungali mdogo.Kubali yaisheBill karibu ningeanguka kiharusi nikifikiri ni wewe umeandika. Kumbe umeidaka kwa mnafiki mlokole Shigingo?? Wataleta kila kitu, wasubiri wapinzani waanze kampeni zao. Shigongo umelipwa ngapi na magazeti yako ya udaku? Njaa tu uzalendo huna!!
Wewe ndiye uliyefumba macho ndiyo maana huoni kama wenzako wamefumba au wamefumbua.Fumbua basi au tumia white stick if any.Haya tena, Shigongo baada ya kugaragazwa kwenye maoni ya CCM anaanza kuleta porojo hapa.
Hivi shigongo unadhani wafanyakazi hamnazo sana ...... unaweza kuwanunua kwa udaku wako????
BMW ntamsifu kwa asilimia 120% lakini kwa JKII imekula kwako. siamini kwasasa tunakula mlo mmoja kwa siku. kwani kukua kwa uchumi ni kupanda gharama ya vyakula? the major human basic need ni kula. sasa kama tathmini inafanyika kwa wafanyakazi na watoto wa ushuani hiyo ni tathmini au ni mtazamo?watu acheni ushabik wakijinga. twende ngaz kwa ngaz. anzia gerezani hadi maofisini. nyumbani hadi kwenye matafrija TOA THATHMINI kwa kulinganisha na kiongozi aliyepita.
KIONGOZI BWM Vs JK
MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009
Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%
unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo 250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500, hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni 120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila waalimu na wenzao.........! 3 years.
Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.
Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.
Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?
Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?
FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona hili wameamua kujicholea MIPAKA yao Mapema.
MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA NA KODI ZENU.
HaaahaTetee,halooo.REV kwa kutukana bwana.ndizo zako tumekuzoea.Powaaa
Siku hiyo ya 31 oct ndiyo utajua si bange
Na Kudhaminiwa na Rev masanilo.Vigezo na masharti kuzingatiwaTANGAZO HILI LIMELETWA KWENU KWA HISANI YA Uday Saddam Hussein al-Tikriti wa Msoga-Chalinze
Vigezo na Masharti kuzingatiwa!
Mgaya juuu.Kura za wafanyakazi kwaaaaa Kikwete.TUCTA safiiiiJana mgaya alitoa tamko na kukana habari iliyoandikwa na TAnzania daima kuwa "TUCTa yamjibu Kikwete"
Kataika gazeti la leo Nipashe Mgaya amesema Jk amesikiliza kilio cha japo hajafikia lengo lao
Mgaya amesema hapo kawajali wafanyakazi kura watampa
Mgaya juuu.Kura za wafanyakazi kwaaaaa Kikwete.TUCTA safiiii