Elections 2010 Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete

Mimi hii habari inatia kichefuchefu sitaki hata kuisoma na hao waliohojiwa nao loh!! kweli maisha bora kwa kila mtanzania aliyehojiwa na kujibu upupu huu
Pole sana.Vumilia tu Baada ya muda hali itakuwa shwari. na utajilaumu kwa nini hukusoma mapema.I wish you all the best
 
Kama source ni global publishers hakuna haja ya kupotez muda kujadili , UMBEA MTUPU
 
Kwanza mwandishi si mtafiti tusimlaumu: Kitaalam sampuli ya wafanyakazi aliowahoji sidhani matokeo yake yanatosha kujumuisha kwa wafanyakazi wote nchini. Pili kusema mishahara imeongezeka ni sawa ila swali dogo la kujiuliza ni kiasi gani cha bidhaa cha nyongeza ya shilingi inaweza kununua. Ukishapata jibu utajua kitaalam hakuna nyongeza yoyote ambayo ni dhahiri....Mungu awanusuru Watanzania kwa vile hata wasomi kama nyinyi waaandishi mnashindwa kujenga hoja....itakuwa kwa wakulima huko vijijini ambao hata hawana mishahara!!!
 

Hii siyo sehemu ya udaku. Pia sitegemei Global publishers watoe kitu kilichokinyume na mkuu wakati juzi katoka kumwomba Shigongo avumilie next term atapata kilichompeleka mwanza.
 
Mmi pia nitampa kura yangu Jakaya mwana wa Kikwete .Anaelezeka.
Tatizo lako ni ufahamu mdogo ulionao. Kikwete anaelezeka vipi? amewadanganya kuhusu ufisadi mnapiga makofi, Hataki kubadilisha katiba mnapiga makofi. Kitu ninacho kiona kwako ni kuwa huna uzalendo wa kweli unachoangalia ni tumbo lako tu, ndo maana unasema kikwete(mafisadi) wanaelezeka. Tafakari sana kwa kina kuhusu nchi yako imetoka wapi na inaelekea wapi. Mambo yanapokuwa mabaya tunawalaumu viongozi, badala ya kujilaumu sisi wenyewe,tunapewa nafasi ya kutafakari na kuchagua viongozi wanaotufaa sisi tunakimbilia CHAMA,HATUTAKI KUFIKIRI.
 
Nia tunayo,elimu tunayo,sababu tunayo.kazi ikiyobaki ni moja tu.TUTAMPA KURA ZETU
Sioni ajabu kusema kuwa utampa kikwete kura, Maana nina amini kitu kimoja watu wanaofaidika na ufisadi wa CCM, wataipigia kura CCM. bila kujali madhala yatakayotupata hapo baadaye kama nchi. Ninakumbuka nilipata kufanya kazi katika Halmashauri moja. Katika halmashauri ile watu walimchukia sana Dr. Silaa(mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa) walikuwa wakisema huyu Silaa ni mtu asiyependa rushwa, hivyo anaharibu ulaji wao. Hao wote najua hawatampigia Kura Dr. Silaa kwama si kiongozi mzuri bali watamnyima kura kwa sababu ni muadilifu.Ndo maana naona wazalendo wa nchi hii ni wachache kabisa.
 
Sishangai watakaompa kura kikwete maana wengi ni wale waliokosa elimu hivyo wakazibwa milango yao yote ya FAHAMU
Nakubaliana na wewe kabisa ndio maana CCM imekuwa ikitamba na kufanya inavyotaka kwasababu wanajua watanzania ni wajinga na ni wavivu kufikiri.
 
Mimi hii habari inatia kichefuchefu sitaki hata kuisoma na hao waliohojiwa nao loh!! kweli maisha bora kwa kila mtanzania aliyehojiwa na kujibu upupu huu
Tatizo kubwa watu wengi sana hawafanyi a realistic country wide evaluation ya situation kisiasa ilivyo nchini.CCM watashinda tu, tena kwa wingi wa kura.
CCM iko madarakani,CCM wanabajeti kubwa,CCM ina wanachama wengi tu mijini na mikoani.Kutegemea chama chochote kingine kushinda is at best wishful thinking!
Ride with the winner.
 
Hao wengine wanaonekana kuwa machagu kule Ohio. "2010 HATUDANGANYIKI"


Shigongo anatuletea machangudoa eti wafanyakazi wamesema, huyu changu kabisa namfahamu hushinda pale kinondoni makaburini, kwa wakazi wa kinondoni tembelea kuanzia saa 2 usiku utamkuta buku tu. HATUDANGANYIKI.
 


Shigongo anatuletea machangudoa eti wafanyakazi wamesema, huyu changu kabisa namfahamu hushinda pale kinondoni makaburini, kwa wakazi wa kinondoni tembelea kuanzia saa 2 usiku utamkuta buku tu. HATUDANGANYIKI.

Naye mfanyakazi na mpiga kura
 
Akili mfilisi kabisa Mandela angesema ride with the winner Afrika kusini isingekuwa hivi leo, ukikata tamaa kata kivyako subiri wengne wakupiganie.
 
Kumbe zile habari za kusema kuwa JK hafai ni uzushi tu, wafanyakazi wanamfagilia.
 
Ni vema kuhoji wafanyakazi kujua wana msimamo gani. Ila wasi wasi wangu mbona umehoji kwenye sector moja tu? Hawa uliowahoji ni manager wa bar na wahudumu wake(bar maids). Kibaya zaidi hawakuwa kwenye akili zao, kwani walikuwa wameshiba offer ya keep change za wateja.

SLAA FOR PRESIDENT 2010, DON'T BE DESEIVED!!
 
Wana JF wala msikonde. Nimepata habari hivi punde kwamba picha za JK alizoanguka Jangwani ziko YouTube. Naomba mwenye nazo a-post nione tafadhali, then nitamjibu Shigongo
 
Akili mfilisi kabisa Mandela angesema ride with the winner Afrika kusini isingekuwa hivi leo, ukikata tamaa kata kivyako subiri wengne wakupiganie.
Sawa Mkuu but you have not argued your case to win this ballot.Mandela na South Africa kwa taairfa yako is another case altogether, the majority was behind Mandela, just as the majority is behind CCM.
Matusi mengi hayajawahi kushinda kura, it just reflects ones stupidity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…