Wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza magari ya volkswagen ya nchini ujerumani waingia kwenye mgomo

Wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza magari ya volkswagen ya nchini ujerumani waingia kwenye mgomo

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen ya huko Ujerumani walianza mgomo mnamo Jumatatu ya tarehe 2 Disemba 2024.
Wafanyakazi hao walianza mgomo kupinga hatua zilizotangazwa na uongozi ambazo ni kupunguza pensheni pamoja na kufunga viwanda vitatu vya kampuni hiyo nchini Ujerumani.

Uongozi wa Volkswagen ulisema kwamba hatua hizo ni za lazima ili kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikumba kampuni hiyo. Ripoti ya fedha ya robo ya tatu ya mwaka 2024 ilionesha kuwa faida ya Kampuni ya Volkswagen ilishuka kwa asilimia 64.
Endapo Volkswagen itavifunga viwanda vyake vitatu vya nchini Ujerumani, familia nyingi zitaathirika kwa sababu Volkswagen ndio kampuni inayoongoza kwa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi nchini humo.

Kampuni ya Volkswagen imejikuta katika hali mbaya ya kiuchumi kutokana na ushindani mkali kutoka nchini China. Vilevile gharama za uzalishaji zimeongezeka katika viwanda vingi vya nchini Ujerumani baada ya nchi zinazounda umoja wa ulaya (EU) kuacha kununua gesi moja kwa moja kutoka Urusi ikiwa ni sehemu ya vikwazo walivyoiwekea nchi ya Urusi baada ya kuanza kwa vita ya Ukraine mwaka 2022.
Chanzo/ Source: DW
"Volkswagen workers strike at factories across Germany – DW – 12/02/2024" Volkswagen workers strike at factories across Germany – DW – 12/02/2024
 
Hawa wazungu wangebaki Tu kwenye combustion engine huku kwenye UMEME mchina amewakaba shingo mno
EU wameweka ukomo wa kutumia combustion engine. After 2035 hawataruhusiwa kununua magari ambayo sio EV . Ila walimchukulia poa mchina, hawakutegemea kama angewapa competition kubwa kiasi hicho. Viwanda ndo vinakufa hivyo Ulaya maana manufacturing country pekee iliyokuwa imebaki ni Ujerumani ambayo inadondoka mdogomdogo kwa kuacha kutumia cheap energy from Russia. Muda huo gesi ya Russia inaenda China. The point of no return, gari la mchina limewaka
 
Back
Top Bottom