KERO Wafanyakazi wa Kampuni ya Lake Lubes ya Kigamboni, Vijibweni tunalipwa chini ya kiwango

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni kuhusiana na agizo la serikali kuhusu kima cha chini cha mshahara kuwa shilingi 308,000. Pamoja na maelekezo hayo kutolewa na kurudiwa mara kadhaa, kuna baadhi ya makampuni bado hayatekelezi kabisa. Mfano, kampuni ninayofanyia kazi—Lake Lubes iliyopo Kigamboni, Vijibweni—hadi leo hawajaongeza hata shilingi elfu kumi.

Bado tunalipwa shilingi 230,000, na juu ya hapo tunakatwa makato kama NSSF. Wakati huo huo, gharama za maisha zimepanda sana—hasa usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Kwa hali ilivyo, fedha inayobaki baada ya matumizi ya lazima ni ndogo sana, wakati mwingine inaishia kugharamia nauli tu.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba serikali imekuwa ikikumbusha mara kwa mara sekta binafsi kufuata viwango hivi vya mishahara, lakini baadhi ya waajiri, hasa makampuni binafsi, hawaonekani kufuata kanuni na miongozo hiyo.

Tunaomba mamlaka husika zilisikie hili na kuchukua hatua. Maisha yamekuwa magumu sana kwa wafanyakazi, na bila utekelezaji wa kima cha chini cha mshahara, hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.
 
Dah chini ya Euro 10,wakati nchi za wenye akili kwa saa sio siku hakuna atakae kubali malipo madogo kihivo. Yaani hiyo 230,000 kwa saa moja. sasa hapo ni mwezi mzima. Inatia kinyaa, nenda Kisemvule viwandani sasa hali ni hiyohiyo..Waliofanikiwa kutowa miwani ya mbao na Kusafiri mnatakiwa kumshukuru Allah. Hapa ni kina Tlaatlaa,wanakura na Kuvimbiwa hawajui nini wabongo wanapitia.
 
Poleni sana. Kwa serikali hii aina time n watanganyika. Tujitetee tu.kwa namna inayo faa.
Kazi ni kipimo cha utu.
 
Aisee hiy
Ni kuhusiana na agizo la serikali kuhusu kima cha chini cha mshahara kuwa shilingi 308,000. Pamoja na maelekezo hayo kutolewa na kurudiwa mara kadhaa, kuna baadhi ya makampuni bado hayatekelezi kabisa. Mfano, kampuni ninayofanyia kazi—Lake Lubes iliyopo Kigamboni, Vijibweni—hadi leo hawajaongeza hata shilingi elfu kumi.

Bado tunalipwa shilingi 230,000, na juu ya hapo tunakatwa makato kama NSSF. Wakati huo huo, gharama za maisha zimepanda sana—hasa usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Kwa hali ilivyo, fedha inayobaki baada ya matumizi ya lazima ni ndogo sana, wakati mwingine inaishia kugharamia nauli tu.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba serikali imekuwa ikikumbusha mara kwa mara sekta binafsi kufuata viwango hivi vya mishahara, lakini baadhi ya waajiri, hasa makampuni binafsi, hawaonekani kufuata kanuni na miongozo hiyo.

Tunaomba mamlaka husika zilisikie hili na kuchukua hatua. Maisha yamekuwa magumu sana kwa wafanyakazi, na bila utekelezaji wa kima cha chini cha mshahara, hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.
Aisee hiyo laki 230k na NSSF wanakata?
 
Back
Top Bottom