DOKEZO Wafanyakazi wa kituo cha usimamizi wa mtandao Maktech(NOC) tunaonewa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baada ya Maktech kukosa tenda ya kituo cha usimamizi wa mtandao (NOC) Cha kampuni ya Vodacom, imetokea sintofahamu baada ya uongozi wa Maktech na Nokia kuwalazimisha wafanyakazi kuandika barua Ya kuomba kuacha kazi ambayo ni kinyume na utaratibu na itapelekea waajiriwa kukosa stahiki zao.

Kituo hicho cha usimamizi wa mtandao kinasimamiwa na NOKIA ambae ndio mkandarasi mkuu na Maktech ambaye ni mkandarasi msaidizi.

Kampuni mpya iliyo shinda Tenda ya uendeshaji itaanza kazi ramsi 1.May.2024 Na moja ya vigezo vilivyo wekwa na NOKIA ni lazima uandike barua ya kuomba kuacha kazi kwa hiari ndio upate ajira kwenye hio kampuni mpya.
Lakini pia mpaka sasa hatujapewa Notice yoyote juu ya ukomo wa Maktech katika uendeshaji

Kwa Hali hii bila Serikali kuingilia Kati tutakosa haki zetu za msingi lakini pia tuna mashaka na Madeni yetu ya muda mrefu ambayo tunaidai kampuni ya Maktech

Tunaomba Serikali na Uongozi wa Vodacom uangalie hili Jambo,
 
Akina Makyao ndo wamekuwa hivi..!!
Nikumbukacho wakati Nokia inawachukua watu wa network toka Celtel, walihamamishiwa straight huko Nokia na kupewa welcome bonus ya mshahara mmoja. Sasa inakuwaje Nokia huyo huyo aliwafanyia hivyo wafanyakazi wake wapya miaka ile, leo yeye ahusike kwenye kuwalazimisha watu kuandika barua ya kuacha kazi kabla ya kuhamia kupya.!?? Wakikuacha je..!??
 
Back
Top Bottom